KUBADILISHA MATUMIZI YA KIWANJA UNAHITAJI MICHORO YA RAMANI.

Viwanja katika maeneo mbalimbali vimepangiwa matumizi na wataalamu wa mipango miji katika wizara ya ardhi kwa namna ambayo wanaona ni sahihi zaidi kitaalamu. Lakini hata hivyo wizara imetoa uhuru wa mtu kuamua kufanya mabadiliko ya matumizi kadiri ya namna alivyoamua kutumia kiwanja chake.

Uhuru wa mtu kufanya mabadiliko ya matumizi ya kiwanja umewekwa kwa sababu ya kasi ya mabadiliko ya kiuchumi na kijamii kwa maeneo husika ambayo yanaweza kuwa yamesababisha mabadiliko ya uhitaji wa huduma husika katika eneo husika.

MTU ANA UHURU WA KIMAAMUZI WA KUFANYA MABADILIKO YA KIWANJA

Hata hivyo mabadiliko haya hayajaruhusiwa kufanyika kienyeji tu, bali mtu anapaswa kupitia mchakato uliowekwa na wizara na kisha kutuma maombi ya mabadiliko ya matumizi ya kiwanja katika wizara ya ardhi.

Moja kati ya mahitaji ambayo mtu anapaswa kuwa nayo ili kutimiza masharti ya kuruhusiwa kufanya mabadiliko ya kimatumizi ni michoro ya ramani ya jengo/majengo ya mradi wa ujenzi ambao mtu ana mpango wa kuujenga katika eneo hilo hivyo anaomba kufanya mabadiliko ya kimatumizi ili apate kibali kinachoendana na matumizi husika ya kiwanja.

NI SHARTI UNAPOTAKA KUFANYA MABADILIKO YA KIMATUMIZI UWE NA MICHORO YA RAMANI YA MRADI UNAOTAKA KUUJENGA

Hii ni kusema kwamba ili mtu aruhusiwe kufanya mabadiliko ya kimatumizi anatakiwa awe yuko katika mchakato wa kuliendeleza eneo hilo, ndio maana hata ada ya kulipia gharama za mabadiliko ya kimatumizi zinatokana na aina na ukubwa wa mradi wa ujenzi unaoenda kujengwa katiaka eneo hilo.

Japo kuna watu ambao hutaka kufanya mabadiliko ya kimatumizi ya viwanja vyao, sio kwa sababu wanataka kuendeleza eneo hilo bali unakuta ana mipango mingine lakini bado masharti ya wizara ni kuwa na michoro ya ramani ili uruhusiwe kufanya mabadiliko kwa sababu wanajua kufanya mabadiliko ya kimatumizi ni kwa sababu ya kuendeleza eneo husika.

UKITAKA KUFANYA MABADILIKO YA RAMANI INALAZIMU UMUONE MTAALAMU WA USANIFU MJADILI MRADI UNAOPELEKEA MABADILIKO HAYO

Ikiwa unahitaji michoro ya ramani kwa ajili ya kufanya mabadiliko ya kimatumizi peke yake tunaweza kuwasiliana kujua namna nzuri ambayo itarahisisha zoezi hilo ambalo huhitaji likusumbue sana kwa sababu pengine mradi husika utakuchukua muda mrefu.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *