HATUA TATU MUHIMU ZA KUANDAA MICHORO YA RAMANI ZA UJENZI NA GHARAMA ZAKE.

Watu wasioelewa kwa undani juu ya mchakato wa uandaaji wa michoro ya ramani za ujenzi huwa na mtazamo wa juu juu sana kuhusiana na utaratibu mzima na mara nyingi hushindwa kuupa mchakato mzima uzito unaostahili kitu ambacho huweza kusababisha kupata huduma duni.

Kwanza mara nyingi karibu kila ramani ya ujenzi huwa na upekee wake, ni mara chache sana mtu unaweza kukuta ramani ya mtu mmoja ikaweza kuendana na mtu mwingine kwa sababu kila mtu ana mahitaji tofauti pamoja na malengo na matamanio tofauti.

Hivyo karibu mara zote michoro ya ramani za ujenzi hupitia hatua hizi tatu muhimu mpaka kukamilika.

Hatua ya kwanza(Preliminary design stage) ni hatua ya kutengeneza wazo na mpangilio na kuuendeleza mpaka kuhakikisha kila hitaji(matumizi ya ndani) limejipanga katika eneo lake kwa usahihi na kwa kufuata mpangilio unaoendana vizuri(zoning) ikiwa ni pamoja na uelekeo sahihi wa jengo(building orientation) kadiri ya matumizi ya ndani yalivyopangiliwa.

HATUA YA KUTENGENEZA WAZO NA MPANGILIO WA NDANI YA JENGO

Hatua ya pili(Scheme design stage) ni kuhakikisha mpangilio husika unaendana na uhalisia wa kiwanja na uhusiano kati yake na maeneo ya jirani pamoja na kutengeneza muonekano wa jengo kwa nje na ubunifu wa paa pamoja na vipengele vingine vya jengo vinavyoboresha muonekano wake.

HATUA YA KUHAKIKISHA UHALISIA UNAZINGATIWA NA KUTENGENEZA MUONEKANO WA NJE

Hatua ya tatu(Final detailed drawings) ni kuandaa michoro ya mwisho ambayo itajumuisha taarifa zote zinazohitajika kwa ajili ya ujenzi kufanyika ikiwa ni pamoja na vipimo vyote vya kila kitu kinachohusika kwenye ujenzi huo pamoja na taarifa nyingine zinazotakiwa na mamlaka zinazohusika na ujenzi kwa ajili ya kupitisha kibali cha ujenzi.

HATUA YA MICHORO YA MWISHO YENYE VIPIMO NA TAARIFA NYINGINE MUHIMU

Katika mchakati mzima kila hatua inagharimu theluthi moja 1/3 ya gharama yote kwa ujumla, yaani gharama ya kazi nzima unaigawanya mara tatu na kila moja inalipwa kwa kila hatua moja ya ujenzi. Hii ni kumaanisha kwamba kama mtu anahitaji hatua ya kwanza peke yake gharama itakuwa ni 1/3 ya gharama kazi nzima.

Karibu sana kwa ushauri.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *