UJENZI NI MAHESABU

Kwa mtu ambaye una mpango wa kujenga ndani ya kipindi cha chini ya miaka mitano ijayo, jambo la kwanza na muhimu unalotakiwa kufanya kwa sasa ni kuanza mchakato. Kadiri unavyoanza mchakato mapema ndivyo kadiri na kufahamu mambo mengi mapema ndivyo unavyopunguza makosa na kurahisisha zoezi hilo.

Unaweza kujiuliza unaanzaje mchakato wakati bado huoni pa kuanzia, ukweli ni kwamba tayari una pa kuanzia na ni vizuri zaidi kama bado hujaanza chochote kwa sababu hiyo inakupa fursa ya kuanza kila kitu kwa usahihi zaidi.

Hata kama huna hata kiwanja wala pesa ya kununua kiwanja, lakini ili mradi uko kwenye mipango basi ni vizuri na sahihi kabisa kwa sababu hiyo ni fursa hadimu zaidi kwako, kwani hapo unachotakiwa kuanza nacho ni ushauri wa kitaalamu. Kabla hujanunua hata kiwanja unatakiwa kupata ushauri wa kitaalamu.

Hivyo baada ya kupata ushauri sasa ndio unatakiwa uanze kwa kuweka mahesabu yako sawa, unatakiwa ucheze na hesabu peke yake kwa kujua utaanza na kitu gani ambacho utakiwekea nguvu mpaka ukitimize aidha ni kwa kununua kiwanja au kwa kuanza kutengeneza michoro ya ramani za mradi wako ili mradi umetengeneza hesabu zako kwa usahihi kuanzia mwanzoni mpaka kumaliza.

Utekelezaji utaanza na hatua ya kwanza ambayo umeiweka kwenye mpangilio huku ukizingatia ushauri wa kitaalamu ulioupata mwanzoni ili kujiepusha na matatizo mbalimbali yanayoweza kujitokeza yanayotokana na uzembe.

Kwa kuweka utaratibu wa kimahesabu namna hii utapata hamasa ya kukamilisha hatua moja baada ya nyingine, jambo ambalo litakuletea furaha na matumaini ya kukamilisha mradi wako badala ya kusubiri ukamilishe mambo bila kuwa na mpango wa kimahesabu unaoufanyia kazi.

Karibu sana

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *