RAMANI NA UJENZI DODOMA

Dodoma ndio mkoa ambao umekuwa na unaoendelea kukua kwa kasi sana kwa kuwa na miradi mingi ya ujenzi inayoanzishwa na kuendelea. Kuanzia serikali ya awamu ya tano ilipoipa kipaumbele sera yake ya kuhamishia ofisi zote za serikali kuu Dodoma, kasi ya mji kukua haijawahi kupungua.

Ofisi mbalimbali na biashara nyingi mpya zimefunguliwa Dodoma na kufanya kasi ya ukuaji wa mji kuwa kubwa zaidi na shughuli za ujenzi kuzidi kushamiri.

RAMANI NA UJENZI DODOMA

Miradi ya ujenzi Dodoma inafanyika kwa ngazi zote kuanzia ngazi ya watu binafsi mpaka ngazi ya taasisi na hasa taasisi za kiserikali ambazo nyingi zimehamia Dodoma na hazijawahi kuwa na majengo ya ofisi Dodoma.

Changamoto kidogo iliyopo Dodoma ni kwenye kupata kibali cha ujenzi, kwa kuwa Dodoma ni makao makuu ya nchi na serikali imeamua kuwa “serious” sana na jiji la Dodoma suala la kupata kibali cha ujenzi limepewa uzito mkubwa na limekuwa linatazamwa kwa umakini mkubwa.

Masharti ya kupata kibali cha ujenzi Dodoma yako tofauti kidogo na miji mingine Tanzania na yamewekewa uzito zaidi na viwango vyake ni vya juu zaidi ya kawaida na ikiwa nyaraka na michoro kwa ajili ya kupata kibali cha ujenzi Dodoma zina kasoro ndogo kabisa basi sio rahisi kukubaliwa mpaka zitimize masharti yote.

RAMANI NA UJENZI DODOMA

Hata hivyo pamoja na kasi ya ukuaji wa jiji la Dodoma kuongezeka sana na miradi mingi ya ujenzi inafanyika lakini bado kuna changamoto kubwa ya mafundi wazuri wanaopatikana Dodoma na mafundi wengi wazuri wanatokea mikoa mingine kwenda kufanya kazi Dodoma.

Karibu ikiwa unahitaji ushauri au msaada wowote wa kitaalamu juu ya ujenzi Dodoma.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

2 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *