RAMANI NA UJENZI DAR ES SALAAM

Dar es Salaam ndio mkoa unaoongoza kwa kuwa na miradi mingi ya ujenzi kuanzia midogo mpaka mikubwa ya watu binafsi, taasisi binafsi, taasisi za kiserikali, miradi ya serikali, taasisi za dini n ahata mashirika ya kimataifa.

Lakini Dar es Salaam ukilinganisha na mikoa mingi sio sehemu rahisi sana ya kufanya ujenzi bila kufuata taratibu zilizowekwa na mamlaka husika. Hata hivyo sio tu kwamba ni vigumu kidogo kufanya ujenzi bila kufuata utaratibu hasa kwenye maeneo ambayo yako mijini sana lakini pia kufanya ujenzi bila kutumia utaalamu unaweza kujikuta umefanya mradi wa viwango duni sana ukilinganisha na majirani zako.

DAR ES SALAAM NDIO MKOA UNAOONGOZA KWA KUWA NA MIRADI MINGI YA UJENZI TANZANIA KUANZIA MIRADI BINAFSI MPAKA YA TAASISI

Kwa upande wa ufundi ukilinganisha na baadhi ya mikoa Dar es Salaam sio sehemu yenye mafundi binafsi wenye ubora sana ukiondoa wale waliofunzwa na makampuni makubwa lakini kwa kuwa siku hizi muingiliano ni mkubwa na usafiri umekuwa rahisi kidogo mafundi wenye ubora kutoka maeneo mbalimbali hufika Dar es Salaam kwa ajili ya kazi na kuondoka, huku wengine wakiloea kabisa.

Kwa bahati nzuri Dar es Salaam ni sehemu inayoongoza kwa kuwa na wataalamu wengi wa masuala yote ya ujenzi kwa ngazi ya kitaalamu(professionalism) kwa sababu kwanza vyuo kadhaa vinavyotoa taaluma za juu za ujenzi vinapatikana Dar es Salaam kwa wingi na wahitimu wanaobaki na kuja Dar es Salaam baada ya kuhitimu masomo ni wengi.

Karibu kwa ushauri, utaalamu au uzoefu wa ujenzi Dar es Salaam.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *