RAMANI NA UJENZI ARUSHA.

Arusha ni moja kati ya majiji yanayokua kwa kasi sana katika sekta ya ujenzi Tanzania. Ni jiji linalojengwa zaidi kaskazini ya Tanzania na kasi ya ukuaji wake ni kubwa sana pia.

Gharama ya vifaa vya ujenzi ni ya wastani ukilinganisha na maeneo mengi ya Tanzania na kwenye suala la ufundi na huduma za kitaalamu watu wanajali sana thamani kulinganisha na gharama ya huduma husika.

ARUSHA NI KATI YA MAJIJI TANZANIA AMBAPO SEKTA YA UJENZI INAKUWA KWA KASI SANA

Arusha ni kati ya maeneo ambapo ambapo mamlaka husika zinafuatilia sana kuhakikisha miradi ya ujenzi ya ngazi zote inafuata sheria zilizowekwa na mamlaka husika kupitia halmashauri ya jiji la Arusha na pia kuna changamoto kubwa ya ufuatiliaji wa vibali vya ujenzi.

Arusha sio eneo lenye usumbufu linapokuja suala la miamba na mawe makubwa ardhini kama Mwanza lakini viwanja vya Arusha mara nyingi huwa ni vidogo sana kwa sababu ardhi inachukuliwa kama kitu cha thamani kubwa Arusha hivyo imekuwa desturi kwa watu kukata viwanja vidogo kuliko kawaida hasa kwa upande wa viwanja vya makazi.

HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA IMEKUWA IKIFUATILIA KWA KARIBU SANA KUHAKIKISHA MRADI YA UJENZI INAFUATA SHERIA ZILIWEKWA NA MAMLAKA

Arusha ni kati ya maeneo ambayo suala la ufundi linapewa umakini mkubwa na ni kati ya maeneo ambayo kuna mafundi binafsi wenye viwango vikubwa vya ubora na ni kati ya majiji ambapo kwa utamaduni watu wanakazana kuhakikisha wanapata huduma bora sana kwa gharama nafuu.

Karibu kwa ushauri wa kitaalamu au ujenzi kwa miradi ya jiji la Arusha.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *