KWENYE UJENZI HULIPII HUDUMA PEKE YAKE ZAIDI UNALIPIA THAMANI.

Imekuwa kawaida kwa watu wengi wanapoambiwa gharama za huduma mbalimbali za ujenzi na hasa huduma za kitaalamu kama ushauri wa kitaalamu na ufundi kupingana kwa kujaribu kulinganisha gharama za huduma hizi kati ya watu na watu.

Kulinganisha huduma kati ya mtaalamu mmoja na mwingine naweza kusema sawa kwa sababu licha ya kwamba watu hawa wanatoa huduma zinazofanana lakini thamani zao ni tofauti, japo kwa bahati mbaya sio rahisi kuona utofauti wa thamani mpaka kazi itakapomalizika.

KWENYE HUDUMA ZA UJENZI KAWAIDA THAMANI NDIO HUAMUA GHARAMA

Watu wengi wanapokuja kufahamu thamani halisi ya huduma na kugundua kwamba walikosea kuchagua huduma sahihi kutofahamu tofauti na huduma hizi hujutia kwa kuona kwamba hawakufanya maamuzi sahihi kwa sababu walikuwa na mtazamo kwamba huduma hizi zina matokea yanayofanana.

Jambo hili huweza kuonekana kwa usahihi pale linapohama kutoka kwenye huduma na kwenda kwenye bidhaa, kwa sababu bidhaa huonekana yote vizuri kabla ya kulipiwa kwa mfano simu janja aina ya Samsung au Iphone ni tofauti sana na simu janja aina ya tecno au feki nyingine zilizopata umaarufu kama feki za kichina.

KULIPIA THAMANI KUTAKUEPUSHA NA MAJUTO ZAIDI KULIKO KULIPIA HUDUMA PEKE YAKE

Hapa ni rahisi mtu kufanya maamuzi sahihi kwa sababu anapima ubora kulinganisha na bei moja kwa moja na hivyo anaona wazi kwamba maamuzi yasipokuwa sahihi atakuja kuyajutia mapema sana. Kwa bahati mbaya kwenye huduma kama za ujenzi wengi huja kujutia baadaye kwa sababu ndipo matokeo huja kuonekana.

Hivyo kila mara unapofanya maamuzi juu ya huduma sahihi ya ujenzi iwe ni ya ushauri wa kitaalamu au ya ufundi ni muhimu kuzingatia mtazamo kwamba unalipia thamani zaidi na sio huduma peke yake. Huduma ziko nyingi ambapo nyingine ni feki na kichina na nyingine ni za uhakika, hivyo unapolinganisha bei ni muhimu kuzingatia kwamba unapaswa kulinganisha na thamani ya huduma yenyewe.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

2 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *