GHARAMA YA UJENZI WA NYUMBA YA GHOROFA

Gharama ya ujenzi wa mradi ndio kitu cha kwanz aambacho kila mtu huwa anafikiria pale anapoanza kufikiria kuhusu kujenga, kitu ambacho ni sahihi kabisa kwa sababu gharama husika ndio inayoamua kama utajenga na kama utajenga ni kwa ukubwa gani au utajumuisha vitu gani.

Kujua gharama ya ujenzi wa jengo lolote kanuni ya kutumia siku zote ni ile ile ya kuchukua ukubwa wa eneo la mita za mraba zinazojengwa na kuzidisha kwa gharama ya kujenga mita moja ya mraba na hapo unapata makadirio ya gharama za jengo zima.

GHARAMA HALISI YA UJENZI UNASABABISHWA NA VITU VINGI VINAVYOTOKANA NA MAAMUZI BINAFSI YA MTEJA

Gharama ya kujenga mita moja ya mraba kwa viwango vilivyowekwa na mamlaka za ujenzi kwa sasa ni wastani wa shilingi za kitanzania milioni moja, inaweza kuongeza zaidi au kupungua zaidi kutegemea na machaguo ambayo mtu anafanya kwenye ujenzi husika hasa kwa upande wa malighafi.

Hata hivyo kwa makadirio ya ufundi wa kawaida kuna vitu ambavyo kwenye ghorofa vinaongezeka ukilinganisha na nyumba ya kawaida ya chini hasa kwa upande wa mfumo wa mihimili ya uimara wa jengo ambao kwa ghorofa hujumuisha vipengele vingi zaidi ukilinganisha na nyumba isiyo ya ghorofa.

KUJADILI KILA KITU KABLA YA UJENZI KUTATOA TASWIRA NZIMA YA GHARAMA INAYOFUATA

Lakini katika uhalisia, ikiwa unahitaji kubana sana bajeti ya matumizi yako katika mradi husika wa ujenzi bila kuathiri viwango vya ubora vya jengo husika unachopaswa kufanya ni kuhitaji mahesabu ya gharama ya malighafi na ufundi yafanyike kisha baada ya hapo kukaa chini na mtaalamu au wataalamu kujadili yale ambayo sio ya lazima ambayo yanaweza kuondolewa na madhara yake kwa kiasi sahihi ambayo yapunguza gharama lakini madhara yakiwa yameshajadiliwa na kudhiriwa.

Karibu sana kwa ushauri.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

21 replies
 1. UWEKEZAJI MAJENGO
  UWEKEZAJI MAJENGO says:

  Asante sana Architect Sebastian,

  Kuhusu milioni moja kwa mita moja ya mraba.

  Na ile kanuni ya kupata gharama za ujenzi kwenye mita za mraba kwenye aya ya pili.

  Kiukweli nashukuru sana kwa maarifa haya.

  Uwe na uandishi wenye mafanikio makubwa.

  Rafiki yako,

  Aliko Musa.

  Real estate investing consultant.

  Reply
 2. Shabani rajabu bakari
  Shabani rajabu bakari says:

  Nikiitaji kujenga nyumba ya ghorofa moja garama yake inaweza fika bei gani? Ujenzi tubila kuweka nakshi zozote ndani.

  Reply
 3. Emma Dominic
  Emma Dominic says:

  Hello.
  Nimefurahia sana uchambuzi wa kitaalamu hapo juu. Mimi naomba msaada, kuna maeneno naona mtu anajenga ghorofa kwa mfumo wa nguzo tu bila tofari mpaka anapaua, kisha anarudi kujenga tofali..naomba kujua kama mfumo huu wa ujenzi unaweza ku save cost! Au mafafanuzi yoyote yanayoweza kunisaidia kuelimika…
  Asante.

  Reply
  • Ujenzi Makini
   Ujenzi Makini says:

   Karibu sana Emma.

   Ujenzi huo haupunguzi gharama bali unaweza kusaidia kufanya kazi kwa awamu hivyo ukawa huhitaji kuwa na pesa yote pamoja.

   Karibu tuwasiliane whatsapp +255717452790.

   Reply
 4. TwiNshi
  TwiNshi says:

  Habari kaka Sebastian!! Nataka kujua Nina ndoto za kujenga nyumba ya ghorofa Moja, yenye vyumba 5 vya kulalia [Master 2], na hayo mabafu yawe classic flan, Sebule kubwa kiasi, choo cha chini, dining room, Jiko, store, Chumba Cha mazoezi {Gym} vifaa sio vingi ni vile basic tu kama 5 hivi, so sio pa kubwa sana, Kiwe kuna uwanja wa Basketball nyuma ya nyumba, etc, gharama inaweza zaidi hiyo million 150?

  Reply

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *