UJENZI WA NYUMBA YA GHOROFA MOJA KWA UPANDE WA MICHORO YA RAMANI.

Kufanya michoro ya ramani kwa ajili ya nyumba ya ghorofa ni tofauti sana na kufanya michoro ya ramani kwa nyumba isiyo ya ghorofa, na utofauti huu haupo kwenye gharama ya michoro ya ramani peke yake bali pia kuna tofauti kubwa kwenye matokeo ya mwisho.

Kwanza michoro ya ramani kwenye ujenzi wa nyumba ya ghorofa imegawanyika mara mbili ambapo kuna michoro ya ramani za usanifu wa jengo ambayo inafanywa msanifu majengo, kisha kuna michoro ya ramani za mihimili ya jeng ambayo inafanywa na mhandisi mihimili.

MFUMO WA MIHIMILI WA NYUMBA ISIYO YA GHOROFA NI RAHISI NA HAINA ULAZIMA WA KUINGIZWA KWENYE MAHESABU YA KIHANDISI

Kwa hiyo licha ya kwamba michoro ya ramani za mradi wa nyumba ya ghorofa ni kubwa zaidi, inayohusisha vitu vingi zaidi na inayohitaji kutumia akili zaidi kuweza kuleta uwiano kati ya ghorofa ya chini na ghorofa ya juu lakini pia inahusisha utaalamu mwingine wa uhandisi mihimili.

Hapo tunaona kwamba sasa gharama ya michoro ya ramani kwa nyumba ya ghorofa inafika angalau mara tatu zaidi ya nyumba ya kawaida kwa sababu licha ya kwamba changamoto yake ni mara mbili ya nyumba ya kawaida lakini ukiongezea na gharama ya michoro ya ramani za uhandisi mihimili gharama yake inaenda angalau mara tatu zaidi ya gharama za michoro ya nyumba ya kawaida.

MFUMO WA MIHIMILI WA NYUMBA YA GHOROFA NI TATA NA KUNA ULAZIMA WA KUINGIZWA KWENYE MAHESABU YA KIHANDISI KUHAKIKISHA UNAFANYIKA KWA USAHIHI

Hata hivyo umakini mkubwa sana unahitajika kwenye kutengeneza michoro ya ramani za nyumba ya ghorofa ili kuhakikisha vipengele vyote vinavyoleta mvuto wa jengo vinapangiliwa kwa usahihi na pia kanda zote zinazoenda kimatumizi ndani ya jengo zinapangilia kwa usahihi ili kurahisisha mzunguko wa watu na vitu ndani ya nyumba husika.

Karibu kwa ushauri wa kitaalamu.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

2 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *