MREJESHO WA MARA KWA MARA WA MAENDELEO YA KAZI YA UJENZI KWA MTEJA NI MUHIMU SANA.

Kwenye mradi wowote ule wa ujenzi sehemu yoyote ile kitu kimoja ambacho ni cha uhakika kwamba lazima kitatokea basi ni makosa mbalimbali ya kiufundi na kitaalamu katika mradi huo. Iwe ni mradi mkubwa wa serikali, iwe ni mradi wa taasisi binafsi au mtu binafsi haijalishi kuna umakini mkubwa kiasi gani makosa ni lazima yatokee.

Ulazima wa makosa kutokea katika mradi wa ujenzi haumaanishi kwamba ndio makosa hayo yaachwe yasitatuliwe, makosa ni kitu cha kwanza kushughulika nacho na kufanya marekebisho mara moja kwa sababu uwepo wa makosa unapunguza ubora na thamani ya jengo husika.

Sasa njia ya uhakika ya kuhakikisha kwamba makosa yanajulikana na kutatuliwa mapema katika kazi ya mradi wa ujenzi ni kupitia kupata mrejesho wa mara kwa mara wa nini kinakwenda vibaya ili kurekebisha mapema kabla kazi haijaendelea mbali na tatizo hilo kuwa vigumu kurekebishika au kurekebishika kwa gharama kubwa sana.

Kupata mrejesho wa mara kwa mara wa maendeleo ya mradi wa ujenzi ili kupata kufahamu mambo ya kuyafanya kazi mapema inapaswa kuwa na mtaalamu msimamizi ambaye anafuatilia kila hatua ya ujenzi kuhakikisha kila kitu kinaenda kama kilivyopangwa.

Msimamizi husika anapaswa kuwa na orodha ya mambo anayoyasimamia na viwango vinapaswa kufikiwa ambayo inakuwa ndio mwongozo kwake wa kupima kama kazi inafanyika katika viwango vilivyokubalika kisha kurudisha mrejesho wa nini hakifanyiki vile inavyopaswa na hatua zinazopaswa kuchukuliwa.

Karibu kwa huduma zote za ushauri na usimamizi.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.  

1 reply

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *