MALIPO YA GHARAMA ZA MICHORO YA RAMANI ZA UJENZI YAENDE SAWA NA KAZI.

Kama tulivyojadili hapo awali kwamba ubora wa kazi na ubovu wa kazi za michoro ya ramani za ujenzi unachangiwa sana na mwenendo wa malipo ya gharama za mradi husika. Kiasi cha malipo kinaweza kuchangia kwa kiasi lakini mwenendo wa malipo ni changamoto kubwa zaidi.

Kwanza kabisa wataalamu wengi kutokana na uzoefu kwenye miradi mingi ambayo huishia njiani bila malipo licha ya juhudi na muda ambazo umewekezwa, wametengeneza hali ya kuwa na mashaka juu ya kama mradi husika uko “serious” au ni sahihi na kitu kinachoweza kuondoa mashaka hayo ni uhakika wa malipo.

Hivyo jambo la kwanza ni kuwepo kwa uhakika wa malipo ambao utaanza kuonekana kwa kufanya mapatano ya uhakika na baada ya kuyagawa malipo kwa mafungu kama matatu basi fungu la kwanza kutolewa baada ya majadiliano ya mwanzoni ya mradi kabla ya kutengeneza pendekezo la kwanza la kazi ya mradi husika.

Hatua zaidi za mbele zitapaswa pia kuendana na malipo husika kwa namna ambayo inahakikisha kuna uwajibikaji wa pande zote mbili.

Hili sio jambo tunazungumza ili kupendelea upande mmoja bali tunazungumza kwa sababu tunafahamu uzito uliopo na ubora wa kazi unaoweza kutokana na uhakika wa malipo katika mazingira ambayo watu wamepoteza uaminifu sana kwa sababu ya uzoefu wa kupata hasara ya muda na hata gharama.

Kila upande unapaswa kuwa na yale inayoyasimamia kuhakikisha mambo yanafanyika kwa usahihi na kwa muda uliopangwa.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

2 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *