CHUMBA CHA MAOMBI, TAHAJUDI AU TAFAKURI KWENYE MAKAZI YA NYUMBA YA KUISHI.

Nyumbani ni moja kati ya sehemu ambazo mtu hutumia muda wake mwingi zaidi kuwepo. Hata kama mtu huyo atakuwa anaenda ofisini au kazini kila siku lakini mara nyingi ataamkia nyumbani na kurudi kulala nyumbani ambapo ndio makazi yake ya kudumu ambapo ndio eneo muhimu la kupumzikia pia baada ya kuchoka na michakato na mihangaiko ya siku nzima.

Kama hiyo haitoshi nyumbani pia ndio eneo ambalo mtu huweka vitu vyake vingi muhimu vya kutumia na kufanya mambo mengine mengi yakiwemo yale ambayo hufanya akiwa nje ya nyumbani.

Na kwa sababu mtu huhitaji utulivu wa nafsi, akili na utulivu wa kiroho ambao mara nyingi anauhitaji nje ya majukumu yake mara kwa mara na eneo hili sio eneo jingine zaidi ya nyumbani.

CHUMBA CHA TAHAJUDI KINAPASWA KUTENGENEZWA NA KUJENGWA KUENDANA NA KAZI YAKE HUSIKA

Hivyo kwa ajili ya utulivu wa nafsi akili na roho ni muhimu mtu kuwa na chumba maalum cha mapumziko hayo sambamba na kufanya mazoezi ya kiakili yatakayompatia utulivu huo wa nafsi na roho anaouhitaji nje ya ratiba yake ya kazi ya kila siku.

Hivyo ni muhimu sana pale mtu anapofikiria kujenga nyumba yake katika hatua ya kutengeneza michoro ya ramani za ujenzi kitaalamu ni muhimu kukawepo chumba maalum chenye utulivu kwa ajili ya mtu kufanya maombi au tahajudi(meditation) au kufanya tafakari ya mambo muhimu ambayo yanamzunguka ili kuweza kufikiria maamuzi sahihi ya kufanya katika maeneo husika.

CHUMBA CHA MAOMBI NA TAHAJUDI KINAPASWA KUWA NA FARAGHA YA KIPEKEE

Chumba hiki kinakuondoa kwenye mzunguko wa nyumba wa kila siku ambao unahusisha watu wote wa ndani ya nyumba ambao hauna eneo ambalo ni utulivu lenye uhakika wa kutoingia mtu kabisa kitu ambacho kinapelekea mtu kushindwa kuwa na muda wa peke yako ambao hakuna mtu yeyote anayeweza kuuingilia kwa sababu yoyote ile.

Karibu kwa kazi nzuri za ushauri wa kitaalamu kwenye ujenzi na namna ya kupangilia kwa sahihi nyumba yako ikijumuisha vitu vyote muhimu kwako kuhakikisha maisha yako yanakuwa bora katika nyanja zote kuanzia kimwili, kiakili na kiroho.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *