MABADILIKO YOYOTE KWENYE UJENZI YAMHUSISHE MTAALAMU ALIYECHORA.

Katika kazi ya kitaalamu ya ujenzi kila kitu ambacho hufanyika, hufanyika kwa kusudi fulani maalum na ambalo ni muhimu sana. Pale ambapo kitu chochote kinataka kubadilishwa kutoka kwenye kazi ya kitaalamu bila kumhusisha mchoraji huja na changamoto yake.

Hivyo huwa ni makosa ambayo huja na madhara yake pale ambapo kazi ya kitaalamu hufanyiwa mabadiliko bila kumhusisha aliyefanya kwa sababu yeye ndiye hufahamu kwa nini ameamua kufanya alichofanya na madhara yake.

Makosa hayo huweza kuwa makubwa zaidi pale ambapo mabadiliko hayo yamefanywa na mtu mwingine lakini ambaye hana ujuzi au utaalamu wa fani ya ujenzi kwani kuna kanuni nyingi muhimu huhusika ambazo sio rahisi mtu asiye kabisa na taaluma husika kuelelewa.

Mabadiliko yanapofanyika wakati wa ujenzi bila kumhusisha mtaalamu mwenyewe aliyefanya kazi husika basi viwango wa ubora wa azi husika huweza kupungua sana kwa namna nyingi sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *