KUJUA WASTANI WA BEI SAHIHI YA UFUNDI WA KUJENGA ANGALIA UWIANO.

Mara nyingi watu na hasa wateja hukosa uhakika wa ni kiasi gani sahihi cha fedha anachotakiwa kulipa kwa ajili ya huduma za ufundi wa ujenzi wa mradi wake na hivyo kuyumbishwa sana na maoni mbalimbali ya watu kama bei aliyochajiwa ni sawa au ni kubwa sana.

Hata hivyo ni kweli kwamba bei hutofautiana kati ya eneo moja na jingine, kwa mfano maeneo ya kijijini unaweza kukuta gharama za ufundi za huko vijijini ni ndogo zaidi ukilinganisha na mijini au gharama za ufundi kwa miji mikubwa ni kubwa zaidi ukilinganisha na miji midogo kwa kuzingatia kwamba soko la huduma hizi ni soko huria.

Lakini licha ya kuwa na soko huria hata hivyo bado kuna wastani wa bei ambayo ndio mtu huweza kuanzia kama kipimo ambacho mtu unaweza kutumia kuanza kupata uhalisia.

Uwiano wa wastani wa bei ya ufundi wa kujenga huchukua asilimia 30% ya gharama za malighafi zote za ujenzi, ambapo kwa wastani huo hiyo gharama huwezi kuongezeka au kupungua kutegemea na vitu vingi lakini kikubwa ni ubora wa ufundi au thamani binafsi ya fundi mwenyewe kwani kila mtu huwa na viwango vyake vya gharama alivyojipangia kwa sababu ni soko huria.

Hata hivyo wastani huo wa bei pale unafanya mahesabu ya gharama zote kwa ujumla za kujenga au angalau nusu moja ya kazi nzima ya ujenzi lakini ikiwa unachukua kitu kimoja kimoja kwa mfano kujenga msingi wa nyumba peke yake, au kupaua peke yake, kuna vipengele vingine ambavyo bei huenda juu zaidi na vingine bei kuwa chini zaidi kwa mfano kupiga ripu bei huwa zaidi ya kawaida.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *