USIMAMIZI SAHIHI WA MRADI WA UJENZI UTAKUEPUSHA NA USUMBUFU, MATESO NA MSONGO WA MAWAZO.

Moja kati ya gharama kubwa ambazo watu huingia bila kujua ni usumbufu na msongo wa mawazo ambao hupitia pale wanapoweka usimamizi usio sahihi kwenye mradi wa ujenzi na mambo mengi kufanyika chini ya kiwango au kusababisha hasara.

Usimamizi sahihi licha ya kukupatia matokeo mazuri sana mwishoni lakini pia hukuepusha kuingia kwenye msongo wa mawazo na makasiriko kwa kazi kufanyika katika viwango sahihi ambapo ubora wa kazi yako hukuletea furaha na ufahari sambamba na amani kubwa ya moyoni.

Hiyo ni sawasawa na mtu kununua bidhaa bora ukilinganisha na kununua bidhaa yenye mashaka, licha ya kwamba mtu anaweza kulipa zaidi kwenye bidhaa bora lakini huwa inampa ufahari na furaha zaidi kuliko bidhaa isiyo na ubora lakini kwa malipo ya chini zaidi ya ile yenye ubora.

Kuna thamani kubwa ya zaidi ya pesa ambayo mtu huipata ambayo ni ya kisaikolijia zaidi tofauti na ya kifedha ambayo huletwa na ubora wa huduma ambayo mtu huwa na shukrani kwa muda mrefu zaidi ya kawaida.

Karibu kwa kazi nzuri za usimamizi zitakazokuepusha na usumbufu, mateso na msongo wa mawazo.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *