IKIWA KUPATA KIBALI CHA UJENZI NI CHANGAMOTO JADILI VIZURI NA MTAALAMU.

Kupata kibali cha ujenzi kwa baadhi ya miradi imekuwa ni changamoto kubwa ambapo mara nyingi kesi ya matumizi ya kiwanja husika ndio imekuwa inaongoza kwa kukwamisha.

Matumizi ya kiwanja yako mengi ya aina mbalimbali na vipengele vidogo ni vingi sana kiasi kwamba ni rahisi mtu kukuta mradi wako haukidh vigezo vya aina ya mradi unaotaka kuujenga.

Sasa ili kuweza kufanikisha suala la kibali licha ya changamoto mbalimbali za mradi na hasa matumizi ya kiwanja unapaswa kukaa chini na mtaalamu wa usanifu majengo na kupanga namna ya kuuweka mradi kwa namna inayoendana na matumizi ya kiwanja lakini pia ikiendana mahitaji yako.

Jambo hili linahitaji kushauriana na kuja na ubunifu ambao unaweza kuendana na kila kinachotakiwa kisheria lakini bila kwenda mbali sana na matumizi ya eneo husika.

Karibu kwa ushauri na mapendekezo zaidi.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *