KAZI NZURI YA KISANIFU NA UJENZI INATAKA MJADALA WA KINA.
Tunapozungumzia kazi nzuri katika usanifu na ujenzi watu wengi akili zao moja kwa moja huwa zinakwenda kwenye muonekano mzuri wenye kuvutia na mpangilio wa mambo kwa muonekano wan je kwa ujumla.
Lakini kazi bora ya usanifu na ujenzi ni zaidi ya uzuri wa muonekano na mpangilio wa mambo kwa nje, kazi ya usanifu na ujenzi inajumuisha vipengele vyote vinavyohusika kwenye ujenzi.
Hata hivyo eneo ambalo hupewa kipaumbele zaidi katika kulihesabu jengo kama lenye ubora ni muonekano wa nje ambao hauhusishi watu wengi zaidi ya mtaalamu mwenyewe, lakini vipengele vingine ambavyo navyo ni muhimu sana vinahitaji ushirikiano na mjadala mpana.
Ubora wa kazi ya usanifu na ujenzi sio ule tu unaozingatia kanuni muhimu za usanifu na ujenzi bali pia unaotoa kipaumbele kikubwa kwa mahitaji, matakwa na matamanio ya mteja katika kufanikisha kile anachotaka kimatumizi na hata kihisia.
Hivyo katika kufanikisha kazi bora ya usanifu na ujenzi inahitaji mjadala wa kina unaomhusisha mtaalamu sambamba na mteja pamoja na wadau wengine mbalimbali wanaohusika katika kutumia jengo husika.
Karibu sana.
Architect Sebastian Moshi.
Whatsapp/Call +255717452790
Leave a Reply
Want to join the discussion?Feel free to contribute!