KILA MWENYE WAZO LA KUJENGA ANAPASWA KUZUNGUMZA NA MTAALAMU WA UJENZI.

Bila kujali hata kama una kiwanja au bado, kama unataka kujenga sasa au baada ya miaka miwili au hata baada ya miaka mitano au hata zaidi ya hapo ni muhimu sana kwa sasa kuonana na mtaalamu wa ujenzi mkajadili kile ambacho unafikiria kufanya kwani itakusaidia kupata uelewa mpana wa mambo mapema n ahata kuanza kufanya maamuzi muhimu mapema.

Kuna vitu vingi sana usivyovijua na unahitaji kuvijua na kuvijua kwako kutakusaidia kufanya maamuzi mengi sahihi na kuepuka hasara ya muda na fedha pamoja na rasilimali nyingine ambazo utakuwa kwenye nafasi nzuri ya kuziokoa kwa kufahamu umuhimu wake mapema kabla hujachelewa.

Unahitaji ufafanuzi mwingi kitaalamu katika usanifu pamoja na ujenzi, lakini pia unahitaji kufahamu michakato mingine ya ujenzi hasa kwenye kupata vibali vya ujenzi kutoka kwenye mamlaka husika ikiwemo kufahamu matumizi sahihi ya eneo na kiasi ambacho unaruhusiwa kufika.

Unahitaji kufahamu kwa wastani kiasi cha gharama za ujenzi na maeneo ambayo yanaongeza sana gharama hizo au kupunguza pamoja na yale yanayowezekana kubadilisha na kufanyika vinginevyo na yale yenye changamoto ili kuamua kwa usahihi zaidi na kitaalamu.

Hivyo suala kwamba unahitaji kuonana na mtaalamu ili kupata mwanga zaidi na ili akusaidie pia kuweza kutambua kile hasa unachohitaji ni suala muhimu sana ambalo unahitaji kulifahamu kwa haraka kadiri inavyowezekana ili kama kuna kuchukua hatua uchukue mapema na kwa wakati sahihi.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *