RAMANI ZA NYUMBA ZA MITANDAONI SIO TATIZO, TATIZO NI KUMPATA ALIYEIFANYA.

Watu wamekuwa wakifikiri kwamba wanaweza kuchukua ramani ya nyumba kwenye mtandao na kwenda kuijenga kwa sababu imeshakamilika. Ukweli ni kwamba ramani za kwenye mitandao ni changamoto sana kama jinsi ilivyo kwa kitu kingine chochote cha kwenye mitandao.

Kwa kawaida mradi wa ujenzi ni vitu vinavyogharimu fedha nyingi na hivyo ukifanya makosa utajikuta unayalipia kwa gharama kubwa kwa sababu hasara zake huwa kubwa sana. Ramani ya kwenye mtandao sio rahisi hata kidogo iweze kuendana na mahitaji yako, kuanzia ya kimatumizi mpaka ya ukubwa.

Hivyo kuchukua ramani ya kwenye mitandao ni rahisi kujikuta ukifanya kitu ambacho hakiendani na mahitaji yako kuanzia ya kimatumizi ya jengo mpaka ukubwa wake ambao utaathiri bajeti yako ya fedha uliyoweka kwa ajili ya mradi husika.

Je hiyo inamaanisha kwamba ramani za kwenye mitandao hazifai?

Kama ramani ya kwenye mitandao huwezi kumpata aliyeifanya na ukaweza kukutana naye ili kuijadili, ndio hiyo ramani haikufai. Lakini ikiwa aliyeifanya ramani hiyo anaweza kupatikana mkaijadili na ikibidi kufanya marekebisho yanayoendana na mahitaji yako basi hapo hakuna tatizo.

Hivyo unapoingia mitandaoni kutafuta ramani ni muhimu zaidi kutafuta mtu aliyeifanya au kutafuta upya kabisa mtu wa kukufanyia ramani kwa sababu huyo utamweleza kila unachotaka na hivyo mtaanza upya kabisa kuipangilia iendane na kile hasa unachotaka tangu mwanzoni kuliko ambayo ilianza kwa lengo tofauti au kwa malengo tofauti ya yule aliyeihitaji.

Watu wengi waliochukua ramani mitandaoni wameishia kujutia sana kwa sababu hasara ambayo mtu anakuja kuingia kwa kugundua kwamba amefanya makosa makubwa au majuto ambayo mtu anakuja kuwa nayo baadaye kwa kuendelea na makosa hayo kwa sababu ya kujaribu kukwepa hasara ni makubwa mara tano mpaka kumi zaidi au zaidi ya hapo ya ile gharama ya ushauri wa kitaalamu ambayo alipaswa aifuate kabla ya kuingiza fedha kwenye ujenzi wa ramani isiyomfaa.

Karibu kwa ushauri wa kitaalamu.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *