NYUMBA UNAYOJENGA KWA RAMANI ZA KUPEWA HAITAKURIDHISHA.

Katika kuridhisha au kusaidia watu wasiojua namna ya kupata ramani au wasio na uelewa juu ya umuhimu wa ramani za nyumba kumekuwa na mazoea ya watu kupewa ramani za nyumba aidha na baadhi ya taasisi au hata na marafiki.

Changamoto kubwa ni kwamba ramani hizi za kupewa sio rahisi kuendana na mahitaji yako, kuanzia matumizi ya ndani mpaka ukubwa wa nyumba yenyewe kwani mara nyingi ni vigumu sana kwa ramani iliyotengenezwa kwa malengo tofauti kuendana na mahitaji yako.

Lakini pamoja na kwamba ni vigumu kwa ramani ambayo haijatengenezwa kwa ajili yako kuendana na matumizi yako binafsi bado katika kujenga itakuhitaji gharama kubwa sawa na ambayo imetegenezwa maalum kwa ajili yako na inayoendana na mahitaji yako.

Hivyo ni muhimu sana kuepuka ramani za kupewa kwa sababu gharama ya kutengeneza ramani ambayo inaendana na mahitaji yako ni ndogo sana ukilinganisha na gharama kubwa unayoingia kujenga kitu ambacho hakitakuridhisha.

Karibu sana

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *