KUONGEZEKA KWA GHARAMA KWENYE UJENZI (VARIATION)

Katika kuomba zabuni ya ujenzi(tendering) kampuni au mtu binafsi huweka gharama ambayo itamwezesha kufanya mradi husika kwa mafanikio sambamba na kupata faida baada ya kuondoa gharama zote za uendeshaji kwa kadiri ya mradi unavyohitaji.

Hata hivyo kutokana na mabadiliko ya mara kwa mara yanayotokana na sababu mbalimbali kubwa ikiwa ni mabadiliko yanayojitokeza wakati mradi unaendelea pamoja na mambo mengine ambayo hayakuweza kufahamika mwanzo kama vile mabadiliko ya hali ya hewa, changamoto ya eneo chini ya ardhi au changamoto nyingine yoyote isiyotegemewa gharama huweza kuongezeka katikati ya mradi.

Hizi ni gharama zisizokwepeka kwa sababu mwanzoni hazikujumuishwa wala kutegemewa kwamba zitatokea na katika kiwango gani hivyo ni jukumu la mteja na mtaalamu aliyepewa kandarasi husika kukaa chini na kukubaliana juu ya mabadiliko hayo na madhara yake kwenye gharama.

Hata hivyo gharama hizi hazitakiwi kuwa ni gharama ambazo zilijulikana tangia mwanzoni ili kuepuka usumbufu, hivyo ni muhimu sana kwamba michoro ya ujenzi husika kumalizika yote na kila kitu kinachohusika kujumuishwa kisha majadala wa kina kuhusu mradi huo, yote yanayokwenda kufanyika, pamoja na viwango vinavyohitajika kujulikana mapema.

Hii itasaidia kupunguza usumbufu katikati ya mradi, kujenga kuaminiana na kuanza kazi katika usahihi unaohitajika hasa upande wa mteja ambao ndio unaohusika kufadhili mradi kifedha.

Karibu sana

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *