MAFUNDI WAZURI WA UJENZI BILA USIMAMIZI SAHIHI BADO INAWEZA KUWA NI KAZI BURE.

Kwenye baadhi ya kazi za ujenzi watu wamekuwa wakishangaa kwa nini mwanzoni waliambiwa fundi fulani ni fundi bora sana na wakati mwingine kuambiwa hata kuna kazi nzuri alifanya lakini bado mwisho wa siku ameishia kuharibu kazi aliyopewa na kuhisi waliahadaiwa na kudanganywa.

Ukweli ni kwamba wakati kweli fundi huyo ni mzuri na kweli anaweza kufanya kazi nzuri lakini mara nyingi inategemea na mazingira ya kazi husika, kwamba huenda kazi nzuri anaweza kuifanya chini ya usimamizi mzuri ndio alete matokeo bora au amepatana kazi kubwa kwa gharama isiyotosha halafu akashindwa kuisimamia kwa usahihi ikaharibika kwa sababu yeye hana uwezo mzuri katika mapatano na usimamizi.

Wakati mwingine unaweza kukuta hana nidhamu ya kazi kwa kujisimamia yeye binafsi na hivyo usimamizi wa utekelezaji, muda na fedha hawezi kusimamia isipokuwa ana uwezo wa kufanya vizuri chini ya usimamizi anapokuwa anabanwa vizuri.

Kuna maeneo ambayo usimamizi sahihi pekee ndio unaoweza kufanya kazi husika katika usahihi unaotakiwa kwa mfano kazi kumalizika kwa muda uliopangwa, usimamizi wa fedha, usimamizi wa ubora unaotarajiwa na utatuzi wa changamoto kubwa mapema kabla hazijawa kikwazo na changamoto zaidi.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *