MAMLAKA ZA UFUATILIAJI WA UJENZI ZINATEGEMEA ZAIDI MAMLAKA ZA VIJIJI.

Mamlaka zinazohusika na kutoa vibali vya ujenzi kama vile halmashauri za miji, manispaa na majiji pamoja na bodi mbalimbali za taaluma za ujenzi kama vile boadi za uhandisi, usanifu majengo na ukandarasi ndizo zenye jukumu la kufuatilia kama mbalimbali inayojengwa imefuata taratibu zilizowekwa na mamlaka husika.

Hata hivyo mamlaka hizi licha ya kujitahidi sana kufuatilia miradi mbalimbali inayojegwa ili kuhakikisha kwamba inapunguza ujenzi holela na wa viwango duni usiofuata taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa sheria bado zina upungufu mkubwa wa wafanyakazi na vitendea kazi na hivyo imekuwa changamoto kubwa kwao kufanya ufuatialiaji madhubuti.

Kiwango cha ufuatiliaji na ukaguzi wa mamlaka hizi bado uko chini sana hata kwa maeneo yaliyopo chini ya mamlaka za halmashauri za miji, manispaa na majiji achilia mbali maeneo ya vijijini au maeneo yaliyopo nje ya halmashauri za miji, manispaa na majiji ambayo ndio ufuatiliaji ni kama hakuna kabisa.

Kutokana na uhaba huo mkubwa wa rasilimali watu wataalamu pamoja na vitendea kazi mamlaka hizi zimeamua kutegemea zaidi mamlaka za serikali za mitaa za maeneo husika kusaidia katika kuhakikisha kwamba miradi husika imefuata taratibu na ikiwa haijafuata taratibu watoe taarifa kwa mamlaka hizi.

Lakini changamoto kubwa kwa kutumia njia hii pia ni kwamba licha ya kutoa mwanya wa vitendo zaidi vya rushwa lakini pia serikali hizi za mitaa hawana watu wenye utaalamu wa kutosha kufuatilia na kutoa taarifa zinazoeleweka juu ya mwenendo wa miradi hii na hivyo inakuwa rahisi aidha kupotoshwa au kutoa taarifa zisizo sahihi huku pia wakiwa hawajui tofauti kati ya mamlaka hizi zinazowatuma.

Hivyo ni muhimu kumhusisha mtaalamu anayeelewa vizuri juu ya sheria na taratibu zilizowekwa na mamlaka hizi ili aweze kudili na watu hawa kwa usahihi na kukuepusha kukuepushia usumbufu usio wa lazima.

Karibu sana

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *