KAZI YA UMALIZIAJI “FINISHING” KATIKA UJENZI HUWEZA KULETA USUMBUFU MKUBWA MWISHONI.

Kufanya kazi yenye ubora siku zote ni jambo bora na muhimu sana, na kufanya kazi isiyozingatia viwango vya juu vya ubora ni rahisi kukutana na matatizo mengi aidha wakati ujenzi unaoendelea au hata huko baadaye baada ya jengo kuwa limeanza kutumika.

Sasa endapo kazi ya ujenzi huko mwanzoni ilikuwa na makosa mengi au mafundi na usimamizi wa kazi husika ni wa kusuasua basi kazi ya umaliziaji “finishing” huweza kuchukua muda mrefu sana na kuja na usumbufu mkubwa sana ikiwemo hata gharama kuongezeka.

Marekebisho madogo madogo huchukua muda mrefu sana na wakati mwingine ukarabati na kujazia maeneo ambayo yalifanyika kimakosa hujitokeza sana japo wakati mwingine kuna maeneo hushindikana kabisa kukaa katika usahihi kutokana na makosa yasiyorekebishika yaliyofanyika huko nyuma kama vile nyumba kukosa mraba(square) iliyokosewa tangu wakati wa kuseti msingi wa jengo.

Hivyo inatakiwa kwanza kabisa nyumba kufanyika kwa usahihi sana tangu wakati wa kuseti msingi wa jengo mwanzoni kabisa mwa mradi lakini pia kuhusisha usimamizi ulio bora na makini sana tangu mwanzoni na hasa katika hatua ya umaliziaji “finishing” ili kazi imalizike kwa haraka kwa viwango vya juu vya ubora.

Karibu sana

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *