KAZI YA UJENZI IWE NA MTAALAMU WA KUIKAGUA NA KUIDHINISHA.

Kwa miradi mikubwa ambayo inafuata taratibu zote za kitaalamu zilizowekwa na mamlaka husika hii sio changamoto kubwa kwa sababu mfumo wa kufanya kazi kitaalamu unafuatwa kwa usahihi na hivyo kudhibiti changamoto zote zinazoweza kusababishwa na udhaifu wa kimfumo.

Lakini kwa miradi isiyofuata utaratibu wa kufanya kazi kitaalamu uliowekwa na mamlaka husika ambayo mingi ni miradi midogo na mingine ya ukubwa wa wastani ni muhimu sana kuhakikisha kunakuwepo mtaalamu mbobezi ambaye ana kazi ya kukagua na kuidhinisha hatua mbalimbali za mradi kwamba ziko sawa na kazi inaweza kuendelea.

Kwa utaratibu huu itasaidia uwajibikaji na umakini kwa upande wa mkandarasi au fundi lakini pia thamani ya kazi inayoendana na thamani ya fedha iliyotolewa kwa kuzingatia kila kilichopangiliwa kinafanyika itakuwa ndio matokeo.

Hilo litakuwa limesaidi pia kupunguza kazi kufanyika kiholela bila kuzingatia muda wala kuwa na viwango maalum vya ubora kwani ni kupitia kuidhinishwa na mtaalamu pekee ndipo kutapelekea kazi kukubalika kwamba iko sawa na inaweza kukubalika.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *