UBORA WA JENGO LAKO UTAONGEZA THAMANI, FURAHA NA HADHI YAKO YA NDANI.

Katika maisha kuna vitu ambavyo havizungumziki lakini tunaweza kuvihisi katika hisia zetu na hisia hizo huwa na nguvu kubwa na kuongeza thamani kubwa katika utajiri wa kihisia. Nafikiri ni kawaida mtu unapokuwa na kitu fulani cha thamani na wewe hujuhisi mwenye thamani fulani na hadhi yako kuongezeka moja kwa moja lakini kitu ambacho utakihisi zaidi katika hisia.

Suala hili la thamani liko kwenye karibu kila kitu kuanzia marafiki wenye thamani utajisikia furaha na fahari kwa ajili yao, ukiwa na mchumba au mke/mume mwenye thamani kwa maana ya tabia nzuri, usafi, akili kichwani, busara, urembo na hadhi nzuri kijamii ni wazi kwamba utasikia furaha na fahari kwa ajili yake, pia ukiwa na gari yenye thamani, simu yenye thamani, mavazi yenye thamani n.k.,

Katika ujenzi pia unapojali thamani na kuipa kipaumbele katika kila hatua ya mradi wako wa ujenzi itakuongezea sana thamani yako wewe ambayo utaihisi kwa ndani, ambapo utajiona kwamba thamani yako imeongezeka na kujiamini kwako kumeongezeka pia na kila unapitazama au kuifikiria nyumba yako unapata furaha au ufahari fulani wa ndani. Ni thamani kubwa ambayo huwezi kuiona wala kuizungumza lakini ukituliza akili unaweza kabisa kuihisi.

Na pale unapofanya kitu kisichokuwa na thamani kama vile kujenga nyumba bila kujali thamani wala ubora wake na ukaona kabisa kitu kilichofanyika hakina hadhi inayokupendeza hilo litakutesa sana moyoni na jambo unaweza kuwa na furaha pia kwa kumaliza lakini bado kuna ukakasi fulani utauhisi kwenye hisia zako kitu ambacho kitakupunguzia ule ufahari wa ndani yako.

Ndio maana utakuta mtu yuko tayari kununua kitu cha hadhi ya juu zaidi ambacho gharama yake ni kubwa zaidi licha ya kwamba kinapatikana kingine cha hadhi ya chini na cha gharama ndogo huku vyote vikifanya kazi ile ile, hiyo ni kwa sababu mtu anatafuta ile furaha, hadhi na ufahari wa ndani ambao unamfanya yeye kuwa na utajiri mkubwa zaidi wa kuhisia unaompa furaha na kujiamini zaidi.

Hivyo ni muhimu sana unapofikiria kufanya ujenzi tangu hatua ya kwanza kabisa kufikiria namna utafanya kazi yenye ubora sana utakaongeza thamani na furaha yako, utakaojivunia na unaoongeza hadhi yako ya ndani pamoja na ufahari ambao utakuongezea sana furaha ya ndani. Hili linaanza kuanzia kwenye huduma ya ushauri wa kitaalamu mpaka ujenzi, vyote viwe ni vya thamani kubwa.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *