CHANGAMOTO NI UFUATILIAJI MADHUBUTI KUTOKA KWENYE MAMLAKA ZA UJENZI.

Kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa na mamlaka za ujenzi, huwa kuna ufuatiliaji wa mara kwa mara wa miradi mbalimbali inayoendelea kuhakikisha inafuata taratibu zote sambamba na kuzingatia kutekeleza kwa usahihi michoro ambayo imepitishwa na mamlaka na kupatiwa kibali.

Utaratibu huu huweza kusaidia katika kuhakikisha kwamba kazi husika inafanyika kwa usahihi na kwa viwango kwa namna ilivyoonekana na kukubalika na idara za ujenzi zinazohusika. Lakini changamoto kubwa iliyopo ni kwamba kuna udhaifu mkubwa kwa upande wa mamlaka kwenye ufuatiliaji.

Hii ni kwa sababu mamlaka karibu zote zina changamoto kubwa ya uhaba wa watendaji ukilinganisha na wingi wa miradi inayoendelea maeneo mbalimbali na kazi kubwa ya kufuatilia kila mradi hivyo utakuta jukumu la kuhakikisha mradi unafanyika kwa kufuata viwango vilivyowekwa linarudi kwa upande wa mteja.

Hata ikiwa kwamba ufuatiliaji wa mamlaka za ujenzi zinazohusika umeboreshwa zaidi bado hakuwezi kuwapo kwa umakini mkubwa sana kwa mradi husika kwa sababu muda ambao wakaguzi wanatumia katika eneo la ujenzi ni kidogo sana ukilinganisha na mambo mengi yanayoendelea na kupita bila kujulikana kama yalifanyika kwa viwango vinavyohitajika.

Hivyo ni muhimu sana kuwa na mtaalamu wa uhakika na anayeaminika ambaye atakuwa na jukumu la kuhakikisha kila kitu kinafanyika kwa usahihi na kwa viwango vinavyokubalika ambaye yuko makini muda wote kufuatilia kila kinachoendelea katika eneo la ujenzi.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *