KWENYE UJENZI UNAHITAJI KAZI YAKO YA KIPEKEE INAYOENDANA NA WEWE.

Imekuwa kawaida kwa mteja kukupigia simu na kuhitaji aone kazi zako ambazo umefanya, kitu ambacho ni sahihi kabisa na muhimu sana katika kujiridhisha juu ya uwezo wa mtu unayetaka kufanya naye kazi. Changamoto huwa ni pale ambapo mteja anakuwa anataka umwonyeshe kazi anayoihitaji na iwe kama anavyotaka yeye iwe akitegemea kwamba unatakiwa uwe nayo.

Kitu ambacho baadhi ya wateja hawajui ni kwamba sio rahisi mtu uwe na kitu anachokihitaji kama kilivyo, ni nadra sana hata kama umefanya miradi zaidi ya mia tano bado utakuta ni mara chache sana kuwa na kitu kinachoendana kwa asilimia mia moja na kile anachokihitaji yeye, kitu ambacho ni sahihi kabisa kwani mtu huhitaji kuwa na mahitaji yanayofanana na wengine.

Baada yake ni kwamba inapaswa mteja anapohitaji kufanyiwa kazi yake anachopaswa ni kujiridhisha na uwezo wa mtaalamu kwa kupitia baadhi ya kazi zake za zilizopita kisha ampatie mahitaji yake na kumtaka amfanyie kazi inayoendana na mapendekezo na matamanio yake binafsi na inayokidhi mahitaji yote yanayoendana na utamaduni wake na mahitaji yake kadiri ya uhalisia wake.

Hivyo sisi wataalamu wa huduma za kitaaluma za ujenzi na ukandarasi tunapokutana na mteja huwa mategemeo yetu ni kumsikiliza mteja anachotaka na kujadili naye kwa kina juu ya yale anayohitaji na namna yataenda kufanyiwa kazi, wakati mwingine kwa msaada wa mifano kutoka kwenye miradi yetu iliyopita kisha kwenda kumfanyia mteja kazi ya ujenzi anayoihitaji ambayo inaendana naye na kumfaa kwa kila kitu.

Kwa maana hiyo huwa hatutegemei kwamba ni lazima tuwe na kazi iliyofanyika zamani ambayo inaendana na mahitaji ya mteja kitu ambacho hata hivyo huwa ni nadra sana kutokea. Kufanya kazi mpya kadiri ya mahitaji mapya ya mteja husika ni jambo ambalo hutupa changamoto mpya na kutusaidia kukua na kutumia uwezo wetu wa kitaalamu uliopo ndani kwa viwango vikubwa.

Hivyo mteja yeyote unaweza kupitia kwenye tovuti yetu hii ya ujenzi makini na ukaingia kwenye kipengele cha miradi, kisha miradi mipya na ukaangalia kazi mbalimbali tulizofanya kuanzia hatua ya michoro ya ramani mpaka hatua ya ujenzi na kuweza kujua uwezo tulionao lakini kwa mradi wako mwingine wa ujenzi tutakufanyia kazi mpya kabisa ambayo itakuwa nzuri kwa namna yake na kwa namna inayoendana na mapendekezo na matamanio yake sambamba na mahitaji yako binafsi.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *