MATUMIZI YA KIWANJA YATAKUPOTEZEA MUDA KWENYE KIBALI CHA UJENZI.

Moja ya kati ya vitu ambavyo ni changamoto kubwa na kero kwa watu wengi kwenye utekelezaji wa miradi ya ujenzi ni pamoja na urasimu ambao mtu huweza kukutana nao kwenye mamlaka za kiserikali katika kufanikisha kusajili mradi wa ujenzi kwa mujibu wa sheria. Na moja kati ya eneo ambalo lina changamoto ambayo huwa iko “serious” sana ni matumizi ya ardhi kwa ujumla sambamba na kwa kiasi umiliki wa ardhi husika.

Changamoto kubwa zaidi iliyopo kwenye matumizi ya ardhi watu wengi kutokuwa na uelewa wa ugumu uliopo kwenye kipato kibali cha ujenzi wa eneo husika unaosababishwa na matumizi ya ardhi husika. Vipengele vya matumizi ya ardhi kawaida huwa ni vingi sana na vingine vinavyokaribiana lakini vikiwa na hadhi tofauti na matumizi tofauti ambapo watu wengi huwa hawajui usumbufu na ugumu uliopo mpaka pale wanapotaka kuanza kujenga wakiwa tayari kwa kila kitu na pale wanapofuata kibali cha ujenzi ndio wanakutana na habari za kuwashangaza.

Mchakato wa kufuatilia mabadiliko ya kimatumizi huwa ni mchakato tofauti kabisa wenye gharama zake tofuati na unaohitaji ufuatiliaji mkubwa na wa karibu. Wakati huo mtu anapokutana na changamoto ya kimatumizi na kuamua kwamba atafuatilia mabadiliko ya kimatumizi ni zoezi linachokuwa muda mrefu na wakati mwingine mradi wake ilipaswa kukamilika kwa haraka zaidi kwa sababu aidha za kiuchumi au kisheria na tofauti nah apo anaweza kuwa kwenye hasara. Hata hivyo muda mali na ucheleweshaji wa namna yoyote ile tayari ni hasara.

Hivyo ili kuepuka usumbufu huu mkubwa ni muhimu sana mtu yeyote unaponunua kiwanja kwa ajili ya matumizi fulani hupaswi kusubiri mpaka utakapoanza kujenga ndio ufuatilie vibali vya ujenzi kadiri ya matumizi ya kiwanja bali ni muhimu kuanza kufuatilia masuala ya kubadilisha matumizi ya kiwanja yaendane na kile unachokwenda kufanya kwenye kiwanja hicho mapema ili unapokuja kuanza kujenga uwe uko tayari badala ya kujikuta unasubiri matumizi ya kiwanja.

Kama wewe una kiwanja ambacho una mpango wa kukiendeleza ni muhimu sasa hivi ukaamua ni nini unataka kujenga katika eneo hilo kisha nenda kwenye mamlaka husika uulize kama unaruhusiwa kwa mujibu wa sheria kujenga hicho unachotaka kujega. Ikiwa unaruhusiwa ni vyema unaweza kusubiri wakati wa ujenzi ukikaribia ukafuatilia kibali cha ujenzi bila shida, lakini kama huruhusiwi kwa mujibu wa sheria kujenga katika eneo hilo ni muhimu sasa hivi ukatuona tukasaidiana kuanza mchakato wa kufanya mabadiliko ya kimatumizi.

Ili itakapofika wakati unataka kuanza kujenga usijikuta ukipitia urasimu mwingi na kupoteza muda wako kuhangaika kufuatilia wakati ukiwa na haraka ya kukamilisha ujenzi pia na hivyo kujikuta kwenye hasara ambayo hukuitegemea.

Karibu sana tufanye kazi pamoja.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *