KUIGA RAMANI YA MTANDAONI NI KAZI NGUMU ZAIDI KULIKO KUFANYA MWENYEWE.

Kuna baadhi ya watu wamekuwa hawaelewi utaratibu wa kazi tunazofanya wala undani wake na kimakosa wamekuwa wanafikiri kazi tunazofanya hususan picha wanazoziona kwamba tunazitoa mitandaoni na kisha kuziendeleza au kuzitumia kama zilivyo. Mtazamo wa aina hii umekuwa ukituweka katika mazingira magumu kwa sababu umepelekea baadhi ya watu kufikiri kwamba kazi tunayofanya ni rahisi sana kwa kuingia tu mtandaoni na kupakuwa kisha kuwapa.

Ukweli ni kwamba hizi kazi hatuchukui mtandaoni bali tunafanya wenyewe kwa kutumia akili zetu, taaluma zetu, maarifa yetu na uzoefu wetu wenyewe. Hii ni kwa sababu kwanza tuna uwezo wa kutosha kufanya kazi wenyewe bila kuiga mahali lakini pia kazi zilizopo mtandaoni sio rahisi hata kidogo kuendana na kile ambacho mteja anahitaji lakini pia kazi hizi mara nyingi huwa hazieleweki na karibu zote hazina vipimo vinavyotosha kuonyesha ukubwa wa jengo hilo.

Kama hiyo haitoshi pia kazi ambayo ipo mtandaoni kuichukua na kujaribu kuiiga ili iendane na mahitaji ya mteja wa mradi husika huwa ni kazi ngumu sana kuliko kazi ambayo mtaalamu anafanya mwenyewe. Yaani kwa kifupi mtu anapoamua kuchukua kazi ya kwenye mtandao ili aitumie kufanya kazi ya mteja hujikuta akiwa na kazi kubwa sana na kupata shida sana katika kuitengeneza iweze kukidhi vigezo na mahitaji ya mteja ambapo ni rahisi zaidi mtu anapoamua kufanya mwenyewe.

Hivyo unapoamua kuamini kwamba kazi zinatoka mitandaoni unakuwa umefikiria kwamba wataalamu wa kazi za michoro ya ramani za ujenzi wanapitia changamoto kubwa zaidi kuliko hata wanavyofanya kazi zao wenyewe bila kufikiria kwamba kuna uwezekano wa kupata kazi hizo mitandaoni.

Hivyo vyovyote inavyokuwa ni kazi ngumu sana inahusika katika kukamilisha michoro ya ramani na hivyo sio sawa mtu anapofikiri kwamba mtu anaweza kutumia njia za mkato kufanikisha kazi yenye thamani kubwa sawa sawa na mahitaji ya mteja wake ambayo sio rahisi kufanana na mteja mwingine yeyote yule duniani.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *