KARIBU UULIZE CHOCHOTE KUHUSIANA NA MASUALA YA UJENZI.

Kama jinsi ilivyo tovuti yetu ni kuelemisha na kutoa ufanunuzi wa mambo mbalimbali katika tasnia ya ujenzi kwa ujumla kuanzia mambo ambayo ni ya kitaalamu, ya kiufundi au hata taratibu nyingine zozote ndani ya taaluma ya ujenzi pamoja na mamlaka mbalimbali zinazohusika kusimamia sekta hii, tunakukaribisha uulize chochote au ufanunuzi juu ya jambo lolote ambalo ungependa ulielewa vizuri zaidi kuhusiana na yote tunajihusisha nayo.

Tunajua kwamba licha ya kuweka makala mbalimbali katika tovuti hii kila siku ambapo tunajitahidi kuzungumzia changamoto nyingi mbalimbali katika sekta ya ujenzi lakini bado sio rahisi kuweza kumridhisha kila mtu au kufafanua changamoto ya kila mtu katika ujenzi, au hata kama tumezungumzia changamoto hiyo hatujaizungumzia kwa namna ambayo mtu anahitaji au kwa kina kiasi cha kutosha kumaliza sintofahamu ya changamoto anayoipitia mtu au hata kama una ushauri wowote kwetu.

Njia pekee ambayo tunaweza kuzungumzia mambo mengi kadiri inavyowezekana na kadiri ya mahitaji ya watu ni kupitia kuwasikiliza wahusika wenyewe na kusikiliza changamoto zao au maswali yao hasa wanachotaka kupata ufafanuzi au, pendekezo au suluhisho juu ya changamoto anayopitia kwani tunafahamu changamoto ziko za aina nyingi sana na karibu kila changamoto una upekee wake unaohitaji kutatuliwa kipekee.

Hivyo sasa tunakukaribisha uweze kutuambia changamoto unayopitia au maswali ambayo huna majibu yake au unafikiria ni wapi sahihi pa kuanzia kushugulika na changamoto hiyo lakini bado uko njia panda, tutakujibu maswali yako au kukusaidia ushauri juu ya changamoto yako kwa kadiri ya uelewa wetu kitaalamu na kitaaluma na kadiri ya uzoefu wetu kwenye changamoto husika na kwa kesi nyingine nyingi ambazo tunashughulika nazo kila siku.

Unaweza kututumia changamoto yako kupitia comment hapo hapo kwenye tovuti ya ujenzi makini lakini kama unapata ugumu kutumia njia hiyo unaweza pia kututumia kwa njia ya whatsapp kwa mawasiliano yaliyopo hapa chini mwishoni mwa makala hii.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *