TOFALI ZA KUCHOMA DAR ES SALAAM.

Kwa sababu mbalimbali tofali za kuchoma zikiwemo za urembo au mazoea na utamaduni tofali a kuchoma zimekuwa zikipewa umuhimu na baadhi ya watu ambao bila kujali upatikanaji wake wamekuwa wakizipa kipaumbele katika miradi yao.

Tofali za kuchoma zimekuwa zikipatikana kwa wingi na kutumika kwa wingi katika mikoa mingi ya hapa Tanzania pengine kutokana na mazoea na kutohitaji teknolojia ya juu sana kuzitengeza. Katika mikoa mingi ya Tanzania tofali hizi zimekuwa zikipatikana isipokuwa mikoa michache sana kutokana na asili ya udongo wa eneo husika.

Dar es Salaam ni kati ya maeneo ambayo tofali za kuchoma ni adimu sana kupatikana kutokana na upatikanaji mkubwa wa mchanga na saruji ambavyo vimesababisha upatikanaji wa tofali za bloku kuwa mkubwa sana kwa sababu ya kukosekana kwa udongo sahihi tofali za kuchoma zimekuwa ni adimu kabisa.

Hivyo kwa mtu ambaye yuko Dar es Salaam na anahitaji tofali za kuchoma kwa sababu ndizo anazohitaji kutumia katika mradi wake wa ujenzi anaotaka kuujenga na anahitaji kwa wingi anapaswa kuagiza tofali hizi kutoka Morogoro ambapo zinatengenezwa kwa wingi katika eneo la Kingolwira.

Nimekuwa nikipigiwa simu mara kwa mara na watu wenye kuhitaji tofali za kuchoma Dar es Salaam ambapo imekuwa ni changamoto kupatikana na kuwapa watu wakati mgumu kwamba ni wapi wanaweza kuzipata. Kwa hiyo kwa kuwa tofali hizi hazitengenezwa Dar es Salaam hakuna budi kuziagiza kutoka Morogoro eneo la Kingolwira ambalo hata hivyo sio umbali mkubwa sana kutokea Dar es Salaam.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *