KUJENGA NYUMBA ZA KUPANGA BILA RAMANI NI KUZIPUNGUZIA THAMANI.
Japo nyumba za kupanga zimekuwa zikilalamikiwa kuwa na kero za aina mbalimbali zinazotokana sababu mbalimbali ambazo nyingi zinazuilika, lakini moja kati ya kero kubwa za nyumba za kupanga hususan nyumba za kupanga Tanzania ni mpangilio mbovu wa nyumba zenyewe. Nyumba za kupanga Tanzania na hasa Dar es Salaam kwa sehemu kubwa zimekosa mpangilio sahihi ambao unaendana na matumizi ya wateja ya kupanga kiasi cha kero na wapangaji kutodumu.
Matokeo ya mpangilio mbovu ni kukosa ushauri sahihi wa kitalaamu tangu mwanzoni na hivyo kupelekea ujenzi kufanyika kiholela bila kuzingatia matumizi ambayo yake na hivyo kugeuka kuwa kero na usumbufu mkubwa kwa wapangaji. Mimi mwenyewe nikiwa ni mhanga ambaye nimewahi kuishi kwenye nyumba ambazo ni kero nimekuwa nikiona wazi makosa yalivyofanyika na kwamba ni kitu gani hakikuzngatiwa mpaka kufikia matokeo hayo ambayo yanaipunguzia nyumba hadhi.
Licha ya faida nyingi sana ambazo ushauri wa kitaalamu na michoro ya ramani kwa nyumba ukijenga kitaalamu zinakuwepo lakini pia ushauri wa kitaalamu na michoro ya ramani ni sehemu muhimu sana ya kuziongezea hadhi na kupunguza kero za nyumba za kupanga hasa ukizingatia uhalisia wa nyumba hizi unavyokuwepo kuanzia mpangilio wa vyumba na nafasi ndani ya nyumba mpaka mpangilio wa maegesho ya magari nje ya nyumba na mahusiano baina ya mpangaji mmoja na mwingine.
Nyumba za kupanga zinapojengwa kwa usahihi na kufuata utaratibu sahihi wa kitaalamu zinaongezeka sana thamani ambayo hata mpangaji mwenyewe anaiona na kuihisi na kutokana na uzoefu wake ataona ni kitu ambacho alikihitaji sana hasa kwenye suala zima la faragha na muonekano.
Kutokana na asili ya nyumba zenyewe za kupanga zilivyo, nyumba za kupanga zinahitaji zadi ushauri wa kitaalamu na michoro ya ramani kuliko hata nyumba za kawaida za kuishi kwani huhitaji mahesabu makali n ahata ukubwa na uwingi wa makazi yenyewe unategemea zaidi ushauri wa kitaalamu kuamua.
Hivyo suala la ubora wa nyumba za kisasa kama matokeo ya kutumia ushauri wa kitaaluma na michoro ya ramani ni suala linaloongeza sana thamani ya nyumba na gharama ambayo ni sahihi sana na muhimu kwani licha ya kumfanya mmiliki wa nyumba kufurahia huduma bora anazozitoa kwa wateja wake lakini pia litamuongezea uhakika wa wateja wa kutegemewa kutokana na ubora wake.
Karibu sana.
Architect Sebastian Moshi.
Whatsapp/Call +255717452790.
Leave a Reply
Want to join the discussion?Feel free to contribute!