NYUMBA YA KAWAIDA KWENDA GHOROFA.

Watu wengi hujenga nyumba zao katika wakati ambao hawana mahitaji makubwa, lakini baada ya muda watu wengi hujikuta wakihitaji nafasi zaidi kwa sababu mbalimbali. Wakati mwingine unakuta ni familia imeongezeka na wakati mwingine utakuta ni mahitaji mengine yameongezeka. Katika nyumba za kupanga wakati mwingine utakuta ni mahitaji yameongezeka sana au wateja zaidi wamelipenda eneo hilo na hivyo kuongeza uhitaji wa ongezeko la ukubwa wa jengo.

Kutokana na mahitaji nafasi zaidi ndani ya nyumba kuongezeka watu wengi wamekuwa wakifanya maamuzi ya kutafuta eneo jingine kwenda kujenga upya nyumba nyingine kubwa zaidi na ile ya mwanzo ni aidha wanaipangisha au kuitumia kwa shughuli nyingine.

Hakuna tatizo kabisa kwenye kufanya maamuzi hayo, na huwa ni maamuzi muhimu sana hasa ukizingatia kwamba watu wengi unakuta kadiri muda unavyoongezeka na kipato chao pia kinaongezeka zaidi na hivyo wanakuwa hawana sababu ya kujibana wakati uwezo wa kuishi eneo lenye nafasi zaidi wanakuwa tayari wanao.

Changamoto ni kwamba watu wanafanya hivyo wakiwa hawana mbadala mwingine, ambapo kama wangeweza kupata mbadala mwingine wa tofauti pengine wangefanya maamuzi hayo.  Hii ni kwa sababu watu wengi wamekuwa wakiyazoea na kuyapenda maeneo wanayoishi na hasa ukizingatia kwamba wanakuwa tayari wameshaimarisha mahusiano yao na majirani na pamoja na watu wengine mbalimbali kama vile huduma za kiroho, hospitali, shule za watoto n.k., na hivyo wasingependa kwenda tena mbali sana kuhamia eneo jipya ambalo watalazimika kuanza upya kila kitu.

Hivyo hawa wanaweza badala yake wakachagua mbadala wa kuwa na nyumba ya ghorofa kwa kuongeza vyumba kwenda juu. Kwa kufanya hivi tayari wanakuwa na angalau mara mbili ya nafasi waliyokuwa nayo katika sakafu ya chini na hivyo kwa wengi wanakuwa wametatua tatizo kwa kiwango kikubwa sana.

Lakini pia kwa kuongeza jengo kwenda juu inasaidia pia kuepuka gharama za kununua tena ardhi nyingine upya huku ukiwa na nyumba yenye hadhi ya juu zaidi kuliko pengine ambayo ungeenda kujenga upya. Kwa maana hiyo hata gharama zinapungua zaidi kwa maamuzi haya.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *