NYUMBA ZA BIASHARA NA UTAALAMU WAKE.

Moja kati ya vitu ambavyo watu wengi hawafahamu ni kwamba watu hupima hadhi zao kutokana na vile vitu ambavyo wanatumia hususan makazi yao. Watu wengi hufikiri kwamba watu hukataa kugharimia vitu vilivyo bora kwa sababu ya gharama peke yake.  Lakini ukweli ni kwamba kitu kikiwa na thamani kubwa watu wengi watajitahidi kujiongeza kulipia gharama zake hata kama na kubwa wa kuangalia ile thamani ambayo wanakwenda kuipata.

Nyumba bora za biashara hususan za kupangisha ni kati ya vitu ambavyo watu hupima hadhi zao kutokana na hadhi ya nyumba ambayo wanaishi na huwa tayari kulipia gharama husika kwa kadiri zinavyoweza kutimiza haja zao za kuonekana wanaishi katika nyumba yenye hadhi ya juu. Nyumba hizi za hadhi ya juu zina utaalamu wake wa kuzitengeneza hasa kuanzia kwenye hatua ya kutengeneza ramani mpaka kuijenga.

Kuna vitu muhimu vya kuzingatia katika kuandaa michoro ya ramani kwa nyumba ambayo inakwenda kuwa bora kuanzia mandhari ya nje, muonekano wake wa nje, mpangilio wake wa ndani na hata aina ya muundo na staili ambayo nyumba husika imechukua. Haya ni mambo ya kitaalamu yanayoiongezea hadhi nyumba kutokana na kazi ya ubunifu iliyofanyika na kuifanya ionekane ni nyumba ya hadhi ya juu inayoweza kumwongezea mteja hadhi yake kimaisha kiasi cha kuwa tayari kulipa kiasi kikubwa cha fedha na kudumu katika eneo hilo ambalo linampa mteja kile ambacho anakihitaji kisaikolojia.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *