NYUMBA YA KUISHI.

Moja kati ya mambo ambayo mtu yeyote anapaswa kuyafanya kwa umakini mkubwa kwa kuzingatia ushauri bora kabisa wa kitaalamu ni pamoja na ujenzi wa nyumba ya kuishi. Hii ni kwa sababu nyumba ni kitu cha kudumu na kwa watu wengi ndio eneo ambalo utaishi maisha yako yote. Jambo hili watu wengi wamekuwa hawalipi uzito unaostahili na hivyo limekuwa likiwagharimu kwa namna nyingi na wakati mwingine kuwaingizia hasara ambazo hawakuzitarajia.

Kwanza kabisa kabla ya kuanza kufanya chochote juu ya nyumba yako ya kuishi unapaswa kujua unataka nini hasa kuhusiana na hiyi nyumba yako ya kuishi. Kisha ukishajua unachotaka hasa unapaswa kujua tena unavitaka kwa viwango gani na kwa wingi kiasi gani. Hilo litakusaidia katika kuanza kuuelewa mradi wako kwa usahihi na yale haswa unayoenda kutekeleza.

Zoezi la kujua kile unachotaka haswa linapaswa kuanza kwa kuangalia pale ulipo sasa ni vitu gani unavitumia na vitu gani ungependa kuwa navyo lakini huna. Hii ni kwa maana ya vyumba au nafasi nyingine ndani ya nyumba unayoishi sasa ambayo unaitumia. Unapaswa kujua vile ambavyo unahisi vinakosekana ambavyo unafikiri vilipaswa kuwepo hapo na vile ambavyo vipo na unavifurahia.

Kisha unaelekea kuangalia vile unavyovipenda ambavyo umekuwa ukiviota mara nyingi au uliwahi kukutana navyo katika maeneo mengine uliyotembelea kama vile, hotelini au kwa Jirani, ndugu au Rafiki au hata ofisini. Baada yah apo utaangalia shughuli zako za kila siku na yale unayoyapa kipaumbele katika maisha yako labda ni sala, au kusoma vitabu au kufanya mazoezi n.k.,

Kwa hivi unakuwa umefahamu vitu vingi unavyohitaji katika nyumba hivyo sasa unaweza kutafuta mtaalamu ambaye mtashirikiana na kushauriana namna vitaenda kuwekwa pamoja kitaalamu na kufanikisha kupata kile haswa unachotaka juu ya nyumba yako ya kuishi. Mtaalamu atakushauri kuhusu mambo mengine na taratibu nyingine za ujenzi kadiri ya taaluma na taratibu zinavyokuwa.

Ukiweza kuweka umakini mkubwa kwenye namna ya kupata nyumba sahihi kwako ya kuishi utaepuka usumbufu mwingi unaotokana na watu kufanya makosa katika kujenga nyumba zao za kuishi na huenda hata ukajikuta hufanyi mabadiliko makubwa baadaye ambayo nayo ni ya gharama kubwa.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *