SAKAFU YA TERRAZO NI YA GHARAMA NAFUU KULIKO SAKAFU ZA VIGAE/FLOOR TILES.

Baadhi ya watu wamekuwa wakifikiria kutumia sakafu mbadala tofauti na vigae vya sakafuni/floor tiles kwenye majengo yao mbalimbali hususan majengo ya taasisi au ya umma wakiwa na sababu mbalimbali. Moja kati ya aina ya sakafu mbadala ambayo watu wengi wamekuwa wakiipendelea zaidi ni sakafu aina ya terrazzo. Lakini kutokana na utamaduni wa kutumia sakafu za terrazzo kupotea sana, watu wengi wamekuwa wakishindwa kujua kuhusu utaratibu wake na gharama zako na hilo kuwaweka njia panda zaidi.

Hata hivyo teknolojia ya terrazzo bado inapatikana na kufanyika hata sasa na inaendelea kufanyika sana. Habari njema kwa watu wanaopendelea kutumia zaidi terrazzo kuliko vigae vya sakafuni/floor tiles ni kwamba kwa sehemu kubwa sakafu ya terrazzo ni ya gharama nafuu kuliko aina nyingi za vigae vya sakafuni/floor tiles. Hii ni kwai le terrazzo kama ya zamani ambayo ni imara sana na ina uso ambao uko rafu kidogo.

Kwa terrazzo za kutumia teknolojia mpya ambazo zimeboreshwa sana na zina uso ambao ni laini kama aina nyingi za vigae vya sakafuni/floor tiles gharama yake iko tofuati. Hata hivyo kwa watu wanaotaka kutumia sakafu ya terrazzo kama mbadala wa kutumia vigae vya sakafuni/floor tiles huwa wanapendelea aina ile lle ya zamani kwa sababu terrazzo zenye uso laini ni kama kurudi tena kutumia vigae vya sakafuni/floor tiles ambazo zina uso laini.

Karibu sana

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

2 replies
 1. Charles selekwa
  Charles selekwa says:

  Habari?
  Mie nimekuwa ni miongoni mwa wengi walio njia panda.
  Nyumba yenye Square meter 160.
  Unaweza kutoa makadirio ya gharama zake nikiamua kuweka tarazo.
  Regard,
  Selekwa

  Reply

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *