MABADILIKO YA MATUMIZI YA KIWANJA.

Moja kati ya changamoto sugu ambazo watu wengi hukutana nazo wakati wanafuatilia vibali vya ujenzi ni suala la matumizi ya kiwanja kuwa tofauti na lengo la mradi unaoombewa kibali. Hili limekuwa tatizo kubwa kwa sababu vipengele vya matumizi ya viwanja vimekuwa vingi sana kiasi kwamba ni rahisi mtu kukuta kile anachotaka kufanya kwenye kiwanja husika hakikidhi vigezo vya kipengele husika cha matumizi ya kiwanja hicho.

Moja kwa moja maamuzi ambayo hufanyika ili zoezi husika liendelee ni kuomba mabadiliko ya matumizi ya kiwanja husika ili kiendana na mradi huo unaoombwa. Na ndipo mtu hulazimika kuanza safari nyingine ya mchakato wa kuomba kubadili matumizi ya kiwanja kupitia halmashauri ya jiji, mji au manispaa husika kisha wizara na ndipo arudi kuja kuomba kibali cha ujenzi upya.

Gharama za kubadili matumizi ya kiwanja inategemea na kile kinachokwenda kufanyika katika mradi huo ambapo huwa ni tofauti kwa kile aina ya mradi na upekee wake. Lakini kwa ujumla kuna hatua tatu za kufuata kufanikisha hili. Kwanza tunaamini michoro tayari ipo kwa sababu ilifanyika ya mwanzoni kabisa kabla hata ya kuanza kufanya kingine chochote.

Kwanza kabisa ni kuweka bango la azimio la kubadili matumizi ya kiwanja husika katika eneo husika la site kwa kipindi cha siku 30 au mwezi mmoja ili kama kuna raia yeyote hakubaliana na matumizi yanayoenda kufanyika basi apeleke malalamiko yake kwenye ofisi za mamlaka husika. Baada ya bango hilo kukaa kwa siku 30 itatakiwa kupeleka katika ofisi za halmashauri ya manispaa husika nakala yake, sambamba na barua ya kuomba mabadiliko ya matumizi hayo.

Itaendelea kesho.

Architect Sebastian Moshi.

Whatasapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *