MABADILIKO YA MATUMIZI YA KIWANJA.

Baada ya kupeleka nyaraka katika halmashauri ya manispaa, jiji au mji husika zinazojumuisha bango hilo na barua ya kuomba mabadiliko ya matumizi utaambatanisha na nakala za michoro ya ramani ya mradi unaoenda kujengwa hapo. Michoro inayotakiwa ni michoro yote inayohitajika ili kazi ya michoro ya ramani iwe imekamilika tayari kwa ajili ya kuanza ujenzi.

Nyaraka hizi zitaandikiwa ripoti na mwakilishi kutoka kwenye idara ya mipango miji kisha faili husika litaingizwa kwenye vikao vya miradi ya ujenzi ambavyo vinakuwa na wataalamu wote wa idara hizo pamoja na mkurugenzi wa halmashauri. Watajadili kila kitu kinachohusu maombi yako mabadiliko ya matumizi kisha kufikia maamuzi na kama wameona hakuna tatizo lolote basi faili hilo litapelekwa wizara kwa ajili ya ukaguzi zaidi.

Huko wizara faili lako litaendelea kuzunguka katika idara zote za halmashauri kama vile idara ya mipango miji, idara ya mazingira, idara ya afya n.k. Watu hao wa wizara wataenda pia kukagua site husika kama imefikia vigezo vya kuruhusiwa mabadiliko. Napo utalipa gharama zilizowekwa kisha wizara itaandika barua ya kuruhusu mabadiliko hayo ya matumizi ya ardhi.

Kisha baada ya hapo unakuwa umekamilisha kufanya mabadiliko ya matumizi ya eneo lako kutoka matumizi fulani kuelekea matumizi mengine. Lakini kama unataka kuendelea na kazi moja kwa moja baada ya kukamilisha mabadiliko ya matumizi sasa unapaswa kurudi kwenye halmashauri na kuomba upya kibali cha ujenzi. Kibali cha ujenzi kitatolewa baada ya kumaliza mchakato mzima na hapo ndio unakuwa unaweza kuanza mradi wako wa ujenzi bila usumbufu wowote.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *