JENGA GHOROFA BILA KUBADILI PAA.

Watu wengi hutaka kufanya mabadiliko ya nyumba zao kutoka nyumba ya kawaida kwenda kuwa ghorofa. Huu ni uamuzi sahihi kabisa na ni uamuzi wa kufanikisha ndoto yako na kufikia mahitaji yako bila kutumia gharama kubwa sana upya ya ujenzi. Lakini kama ulitumia vigae au “havy tiles” katika upauaji wa paa la juu unaweza kuwa na faida zaidi.

Faida hii ni kuweza kung’oa paa hilo kwa umakini mkubwa na kuja kuliweka tena juu ya paa jipya badala ya kulibomoa na kuliharibu lote. Hii ni kazi inayowezekana lakini inayohusisha utaalamu na ufundi wa hali ya juu sana katika kulifanikisha bila paa la zamani kuvuja au kuwa na uharibifu mwingine utakaolipelekea kushindikana kufaa tena kwa matumizi.

Ahsante sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *