KWENYE HUDUMA ZA UJENZI UNALIPIA MUDA NA USUMBUFU.

Moja kati ya maeneo ambayo watu wengi ambao hawaelewi vizuri thamani ya muda na utaalamu huwa hawajali kuhusu uzito wake ni katika eneo la ufundi na utaalamu. Watu wengi huona kama mtaalamu au fundi anayelipwa kwa kazi za kiufundi au kitaalamu analipwa pesa nyingi sana ambazo pengine hastahili. Hili huweza kuonekana wazi pale unapokuta mteja anaweza kuwa tayari kutumia pesa nyingi sana kununua vifaa vya ujenzi vyenye ubora wa hali ya juu sana lakini asiwe tayari kulipa kiwango cha fedha za huduma zenye ubora za kiufundi.

Wateja wengi huona kama wanaibiwa au wanalanguliwa kwa kutajiwa bei za kiufundi au za kitaalamu kwa sababu wanachoangalia sio ubora wa huduma ile au utaalamu husika bali wanaona kama ni pesa inayotolewa bure kwa mtu. Wanachosahau ni kwamba hata thamani ya ile bidhaa ambayo wako tayari kutumia pesa nyingi sana kuinunua katika ubora ina thamani sawa na muda sambamba na utaalamu unaoenda kutumika.

Matokeo yake ni kwamba watu wengi ambao huwa wanakosa umakini katika kutazama jambo hili huishia kupata huduma mbovu isiyoendana na thamani ya vifaa bora walivyonunua. Utakuta vifaa vya bei ghali vimetumika kujenga nyumba kwa viwango duni vya kiufundi na hilo linasababisha jengo husika kukosa ile thamani haswa iliyokusudiwa.

Jambo la msingi sana na muhimu la kuzingatia ni kufahamu kwamba kazi yoyote ili iwe nzuri inahitaji usimamizi makini na thabiti. Usimamizi makini unatokana na mtu mwenye uwezo mkubwa kiutalaamu na mwenye uzoefu ambaye kwa vyovyote ametumia muda mwingi kufikia uwezo huo wa juu. Mtu huyo ndiye atakayetumia muda wake huo katika mradi husika na kuvaa jukumu la kuhakikisha inatolewa huduma bora sana ya viwango vya juu ambayo itafanikisha kupata thamani ya juu iliyokusudiwa.

Usimamizi wa mtaalamu huyu unamuepushia mteja usumbufu mkubwa na kuokoa muda wake ambao ataupeleka kwenye mambo mengine na kwa baadaye unamuepusha mteja na hasara kubwa inayoweza kutokana na ufundi mbovu. Haya ni mambo ambayo kwa kanuni ya asili peke yake hayawezi kupatikana kiurahisi bila kuhusisha watu wenye uwezo mkubwa lakini wenye muda mchache.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *