URASIMU NI MKUBWA SANA KWENYE KUSAJILI MRADI WA UJENZI KUWA MJANJA.

Moja kati ya vitu huwa vinachelesha sana miradi mingi ya ujenzi kuanza hasa miradi mikubwa ni pamoja na urasimu mkubwa uliowekwa ambao unapaswa kufuatwa ili kukamilisha usajili. Hii ni kwa sababu pia changamoto pekee ya kusajili haipo kwenye wingi wa hatua za kufuata kukamilisha mchakato bali hata kwenye muda ambao unatumika kukamilisha hatua moja kwenda hatua nyingine.

Hivyo ikiwa una mradi wa ujenzi ambao una haraka na ungependa mambo yote hususan ya usajili yafanyika kwa haraka zaidi ili kukamilisha kazi mapema basi unahitaji kuhakikisha unakaa chini na watu wenye uzoefu wa miradi hii na kuangalia namna kazi hiyo inaweza kufanyika kwa njia sahihi zaidi. Hili ni jambo muhimu sana kwa sababu utakutana na mambo mengi yatakayochukua muda mrefu sana tofauti na ulivyotegemea na hilo litakuletea changamoto kubwa ikiwa kuna ulazima wa mambo kwenda haraka.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *