GHARAMA YA KUKWEPA UTAALAMU KWENYE UJENZI.

Nimekuwa nikilala kwenye hoteli mbalimbali ninaposafiri kwenye mikoa tofauti na hilo limenpa fursa ya kujifunza mengi yanayohusiana na fani yangu ya usanifu majengo na ujenzi kwa maeneo ninayofikia. Licha ya kwamba watu wengi wanajitahidi kujenga kwa viwango vizuri ili kuvutia wateja lakini unaweza kuona wazi jinsi watu hawa wanatumia pesa nyingi ambazo wangeweza kuziokoa na kufanyia mambo mengine.

Kwa mfano nimekuwa nikiangalia ukubwa wa vyumba vya hoteli au lodge ambazo ninazofikia ambapo kuna ambazo zina nafasi kubwa sana ndani isiyohitajika kwa vyovyote vile na mtumiaji. Ukubwa huo unaongeza sana gharama ya ujenzi kwa kiasi kikubwa kama ilivyo tu kujenga nyumba. Lakini ukubwa huo mara nyingi unatokana na kukosekana kwa elimu ya kutosha kwa yule aliyefanya kazi au aliyeshauri kazi ifanyike kwa namna hiyo.

Hivyo kama mtu anategemea kurudisha fedha yake na faida kupitia wakaaji wa nyumba itamchukue muda mrefu sana kwa sababu alijenga nyumba kubwa sana isiyo na ulazima. Hivyo umuhimu wa mtaalamu kwa eneo kama hili ndio muhimu sana ili kukuepishia na uwezekano wa kuingia gharama kubwa isiyo na sababu.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *