JENGO NI KAMA MJI, NI KITU KINACHOBADILIKA KWA KWA MUUNDO NA MATUMIZI.

Moja kati ya vitu ambavyo huwa vinabadilika kwa kasi sana basi ni pamoja na mipango ya mtu katika maisha. Ukitaka kujua hili kiusawa sawa unapaswa kuanza kuandika mipango yako kuanzia leo halafu kila baada ya miaka mitatu mpaka mitano uje upitie mipango yako ya nyuma. Utashangazwa na vile umebadilika unaweza kufikiri sio wewe, yaani unaweza kudhani yule aliyekuwa anapanga mipango hiyo ni mtu mwingine kabisa. Na hii ndio nguvu ya mtazamo, pale mtazamo wa mtu unapobadilika na akaanza kuamini vingine basi vile vya nyuma huonekana kama havifani na vimepitwa na wakati na hivyo kubadilishwa.

Hivyo ndivyo ilivyo hata kwenye suala zima la ujenzi. Japo kweli kuna watu huwa wana msimamo mkali sana ambao sio rahisi kubadilika lakini kuna wakati suala la kubadilika linakuwa ni la lazima kutoka na uhalisia wa mambo ulivyo kwa wakati husika. Hivyo ndivyo ilivyo kwa majengo tunayojenga. Majengo tunayojenga hufikia mahali na kuhitaji mabadiliko kwa sababu mbalimbali za kimuundo na kimatumizi. Jengo linaweza kufikia kuhitaji mabadiliko ili lionekane kuwa na mvuto zaidi au kuhitaji mabadiliko kwa sababu matumizi yamebadilika au yameongezeka.

Hivyo pale tunapokuwa tunafanya kazi ya kutengeneza michoro ya jengo kwa mara ya kwanza ni muhimu sana kufikiria kama kuna mpango wowote wa mabadiliko ya kimuundo na kimatumizi hapo baadaye. Lakini hata kama haipo kulingana na asili ya jengo lenyewe au aina ya taasisi inayokwenda kufanya bado ni muhimu kuweka matarajio hayo kwani kesho huwa haijalikani itakuwaje. Hili litasaidia katika kutengeneza ramani ya jengo ambayo itaweza kuendana na mabadiliko yanayotazamiwa au kukisiwa.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *