JENGO NI MPANGILIO WA NAFASI ZA KIMATUMIZI(SPATIAL ORGANISATION)

-Unapoliangalia jengo kwa nje kama sio mtaalamu wa masuala ya majengo unaweza kujiuliza maswali mengi sana y ani namna gani jengo hilo limefikia hapo lilipofikia. Kuna mtu mwingine anaweza kufikiri kwamba limefikia hapo kwa kanuni rahisi na mwingine akafikiri limefikia hapo kwa kanuni tata kutegemea na mtazamo na uelewa tofauti wa kila moja. Lakini tafsiri hasa ya jengo ambayo inaweza pia kuanza kuleta picha ya ni namna gani jengo limefikia hapo lilipofikia ni kwamba, jengo ni mpangilio wa nafasi za matumizi ndani ya jengo husika.

Yaani kinachoonekana ni matokeo ya mpangilio uliokusudiwa wa kimatumizi ndani ya jengo hilo na mpangilio wa kimatumizi ndio umeathiri matokeo ya vyote vinavyoonekana kwa nje. Naweza kusema kwamba matokeo ya mpangilio sio ya kanuni rahisi bali ni ya kanuni tata kwa namna yoyote ile kwa sababu mpangilio huo wa kimatumizi unaletwa na mahusiano baina ya matumizi yenyewe ya nafasi hizo ndani ya jengo. Yaani kuna uhusiano mkubwa unaotakiwa ambao unaweza kuwa ni uhusiano wa matumizi kwa uelekeo mlalo au uhusiano wa kimatumizi kwa uelekeo wa pande zote wima na mlalo ambao unaathiri sana matumizi ya nafasi hizo ndani ya jengo.

Pale uhusiano wa kimatumizi unapokuwa haujazingatiwa iwe ni kwa uelekeo mlalo au kwa ulekeo wa wima na mlalo matokeo yake ni kwamba mtumiaji ndiye atakayepata usumbufu wakati wa kutumia. Kwa kawaida uhusiano wa nafasi za matumizi ndani ya jengo ukizingatia kwa umakini humuondolea usumbufu mtumaiaji au watumiaji wa jengo hilo na hata kufanya maisha ndani ya jengo hilo kuwa rahisi na yenye kuendana vizuri na mizinguko ya watu na vitu ndani. Hili ni jambo muhimu sana kuzingatiwa katika kutengeneza ramani ya jengo lolote au eneo lolote.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *