HOWARD ROARK ANAPEWA KAZI YA UJENZI NA AUSTEN HELLER

1. Howard Roark anarudi kwenye ofisi ya John Erik Snyte kuchukua vifaa vyake vya kazi. Anamwambia John Erik Snyte kwamba alisaini mkataba na Austen Heller.

2. Mr. John Erik Snyte anajaribu kumshawishi Howard Roark alete huo mradi ofisini wagawane faida kisha aendelee kufanya kazi ofisini hapo kwa kupandishwa zaidi mshahara kwa sababu hata kazi ameipatia ofisini hapo lakini Howard Roark anamkatalia kabisa.

3. Mr. John Erik Snyte alijaribu kumshawishi sana Howard Roark lakini alikataa kabisa mpaka akafikiria kumfungulia mashtaka ila akaahirisha.

4. Peter Keating anamtembelea Howard Roark ofisini kwake na kushangaa kwamba amefanikiwa kufungua ofisi yake mwenyewe.

5. Wanazungumza ofisini kwa Howard Roark kwa muda mrefu sana juu ya yeye kufungua ofisi hiyo na kama atafanikiwa kupata usajili japo Peter kuna wakati anahisi kama kutofurahishwa na hilo.

6. Howard Roark anaenda New Jersey kuonana na Henry Cameron kumweleza juu ya suala la yeye kufungua ofisi yake mwenyewe na kisha Henry Cameron anampa ushauri mrefu sana.

7. Howard Roark anakamilisha hatua ya design ya mradi wa Austen Heller na kisha kutafuta mkandarasi wa kuujenga. Howard Roark anapata changamoto ya kupata mkandarasi kwani wakandarasi wengi wanamkatalia kutokana na utata wa mradi wenyewe.

8. Mwishoye Howard Roark anafanikiwa kupata kampuni ndogo ya ukandarasi ambayo inakubali kufanya mradi kwa sababu pia ina uhaba wa miradi chini ya usimamizi wa Howard Roark mwenyewe.

9. Austen Heller anatembelea ujenzi wa nyumba yake mara kwa mara na kuuliza maswali mengi kwa Howard Roark. Howard Roark anamwambia Austen Heller kwamba nyumba yake ni kama mtu, kila kipengele alichoweka kwenye design kina kazi muhimu, yaani hakuna mbwembwe zisizo na matumizi.

10. Baada ya ujenzi wa nyumba ya Austen Heller iliyofanywa na kujengwa na Howard Roark kukamilika watu wengi wamekuwa wakiishangaa. Wanataaluma wengi wa kwenye fani ya Usanifu Majengo wameikosoa na kuikejeli sana. Ralston Holcombe amefikia hatua mpaka ya kutaka mamlaka husika kutoruhusu ujenzi wa nyumba kama hiyo. Anasema ni aibu sana kwa taaluma nzima ya ujenzi.

11. Dominique anafanya kazi kwa karibu na Alvah Scarret. Alvah Scarret anampa Dominique kazi ya kufanya utafiti wa kina juu ya maisha ya uswahilini(slums). Dominique anahamia kabisa huko kwa muda kwa ajili ya utafiti.

12. Alvah Scarret na Dominique wanaongea na Dominique anamshangaza Alvah Scarret kwa kutokuwa na kitu chochote cha maana kinachomvutia.

13. Guy Francon anajaribu kuwakutanisha tena Peter Keating na Dominique. Guy Francon anaondoka haraka anawaaga akijifanya ana appointment na kumwacha binti yake Dominique akiwa na Peter Keating.

14. Safari hii Dominique ameamua kumpa ushirikiano mkubwa Peter Keating. Wanaelewana zaidi na kukutana mara kwa mara sana.

15. Peter Keating anarudi nyumbani kwa mama yake. Catherine anakuja mbio na kumwambia Peter kwamba anataka amuoe haraka, amuoe kesho kwamba sababu amepata woga na wasiwasi mkubwa hivyo anahitaji amuoe. Catherine alielezea kwamba amepata hofu na mshtuko mkubwa na anahitaji ndoa. Peter Keating anamkubalia kwamba wataoana kesho yake na Mrs. Keating, mama yake Peter Keating anasema hana pingamizi.

16. Catherine anaondoka kurudi nyumbani.

17. Mama yake Peter Keating anamwambia Peter kwamba hawezi kumwamulia mwanamke wa kumuoa lakini ajue kwamba anaenda kuharibu kazi yake kwa sababu ya kutofanya maamuzi sahihi juu ya ndoa kwa kuoa mwanamke wa hadhi ya chini.

18. Mrs. Keating anamkumbusha Peter kwamba Guy Francon anataka Peter amuoe binti yake Dominique hivyo atasikitika sana akigundua kwamba ameoa mwanamke mwingine.

19. Mama yake anamkumbusha kwamba Guy Francon anataka kumfanya mshirika kwenye kampuni yao lakini atakaposikia ameoa binti mwingine badala ya binti yake basi anaweza hata kumfukuza kabisa kwenye kampuni hiyo licha ya kumfanya mshirika.

20. Mrs. Keating anamwambia Peter kwamba ni jambo la kusikitisha sana yeye kutojijali na kujithamini kiasi cha kwenda kuoa kibinti cha mtaani kisichoeleweka wala kusoma ambacho kinaweza hata kumtia aibu mbele za wageni wa heshima.

21. Peter Keating hafurahishwi na jinsi mama yake anamzungumzia Catherine na hakupendi azidi kumdhihaki.

22. Mama yake Peter baada ya kuongea usiku kucha anafanikiwa kumshawishi Peter kusubiri angalau kwa miezi kadhaa mpaka atakapofanikiwa kuwa mshirika wa Guy Francon badala ya kukimbilia kumuoa Catherine haraka haraka na kujiweka kwenye wakati mgumu kazini.

23. Peter anaenda kumuona Catherine kesho yake na kumwambia kuhusu kusubiri kidogo na Catherine anakubali na hata yeye mwenyewe alifikiria hivyo.

24. Mrs. Wayne Wilmot anafika ofisini kwa Howard Roark akihitaji kufanyiwa design ya nyumba kama Tudor house. Howard Roark anajaribu kumshawishi kwamba anahitaji nyumba ya kupekee kwa ajili yake badala ya kwenda ku-copy Tudor house ambayo ilijengwa kwa makusudi mengine. Mrs. Wayne Wilmot anakataa na kwamba anahitaji hiyo hiyo kwani watu wanaizungumzia na ni nzuri inakubalika. Mwisho Howard Roark anamwambia Mrs. Wayne Wilmot atafute mtu mwingine yeye hawezi kufanya hiyo kazi ya namna hiyo. Mrs. Wayne Wilmot aliyependekezwa kwa Howard Roark kupitia kwa Austen Heller anasema kwamba alionywa mapema kwamba hatawezana na Howard Roark.

25. Mr. Robert L. Mundy anaunganishwa kwa Howard Roark na Austen Heller. Mr. Robert L. Mundy ni mtu mwenye pesa sana na hajali gharama lakini anataka nyumba kama Randolph house. Howard Roark anajaribu kumshawishi afikirie vizuri aweze kupata nyumba yake ya kipekee kwani hiyo Randolph ilikuwa imelengwa tofauti na yeye. Mr. Robert L. Mundy anamwambia amekuwa na mipango ya muda mrefu sana ya kujenga nyumba hiyo na anaihitaji hiyo hiyo kwa sababu ndio anayoipenda. Hivyo Howard Roark alikataa kazi yake.

26. Mr. Jans anaunganishwa kwa Howard Roark ambaye baada ya kumshawishi sana kwamba jengo sio lazima lifanyike kwa namna ya kuwapendeza watu(wananchi) anakubaliana naye lakini mapendekezo ya Howard Roark yanakataliwa na bodi ya wakurugenzi ya kampuni ya majengo ya Mr. Jans.

27. Gowans anampa Howard Roark mradi wa kufanya kituo cha mafuta ambapo licha ya watu kumkosoa sana kwa kumpa kazi Howard Roark lakini anajifanya hawasikii na Howard Roark anafanya kazi hiyo mpaka kuimaliza.

28. John Fargo naye anampa Howard Roark naye kazi ya kufanya design ya maduka moja kwa moja baada ya kutembelea kazi zake mbili.

29. Mr. Whitford Sanboard anampa kazi Howard Roark ya kufanya design ya nyumba yao baada ya kupendekezwa na Henry Cameron. Nyumba hiyo inapata ukosoaji mkubwa kutoka kwa familia hususan kutoka kwa mke wa Mr. Whitford Sanboard isipokuwa mtoto wao wa kiume. Mr. Whitford anapata msukumo mkubwa kutoka kwa familia juu ya Howard Roark.

30. Mwisho nyumba inakamilika lakini mke wa Mr. Whitford Sanboard anagoma kuishi kwenye nyumba hiyo na kuondoka kwenda Vacation Florida. Jarida la Architects Guild of America linaripoti juu ya nyumba iliyotelekezwa na familia baada ya kufanywa na Howard Roark.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *