PETER KEATING ANAMTISHA LUCIUS HEYER ANAPATA MSHTUKO NA KUFARIKI KISHA ANARITHI HISA ZAKE ZA KAMPUNI YA USANIFU MAJENGO

KITABU: FOUNTAINHEAD.

AUTHOR: AYN RAND.

1. Lucius Heyer hakufariki kwa urahisi kama ilivyotegemewa, ameweza kupona na kurudi tena ofisini.

2. Guy Francon anataka kumnunua Lucius Heyer, lakini Heyer anakataa.

3. Kampuni ya Francon & Heyer inaingia kwenye ushindani wa mradi mkubwa wa jengo lenye mvuto zaidi duniani.

4. Henry Cameron anamwita Howard Roark nyumbani kwake New Jersey. Ndio kwa mara ya kwanza Henry Cameron kumwita Howard Roark.

5. Henry Cameron anaongea na Howard Roark kuhusu mambo mengi sana ya kuhusu kazi yake na kumpa ushauri juu ya mambo mbalimbali. Anamwambia awe makini sana na Gail Wynand, anasema Gail Wynand ndiye mtu mwovu zaidi duniani.

6. Henry Cameron anafariki siku chache baadaye. 7. Peter Keating na Dominique wanaendelea kutoka outing mara kwa mara zaidi. Peter Keating anamwambia Dominique kwamba anampenda sana na amechanganyikiwa juu yake.

8. Dominique anamwambia Peter, ikiwa yeye binafsi Dominique anataka kujiadhibu vikali na kujidharau sana, basi atamuoa Dominique.

9. Peter anamwambia Dominique anamwomba akubali kumuoa kwa masharti yoyote yale.

10. Peter Keating anatamani Lucius Heyer afariki ili aweze kurithi nafasi yake ya ubia katika kampuni ya Francon & Heyer.

11. Licha ya daktari wake kuonya kwamba Lucius Heyer atapata stroki ya pili ambayo itamdhoofisha zaidi na kumlaza chini lakini Heyer hakufariki wala hajakata tamaa.

12. Peter Keating anamtembelea Heyer nyumbani kwake kujaribu kumshawishi aachie ngazi kwenye kampuni lakini Heyer anasema yeye bado yuko vizuri na hayuko tayari kuachia umiliki wake.

13. Peter Keating anamtishia Heyer kwamba atapeleka taarifa zake kwenye bodi yenye mamlaka ili afutwe kwa sababu kuna taratibu hakukamilisha. Lucius Heyer anamwomba sana Peter Keating asifanye hivyo na anaamini kwamba yeye ni kijana mzuri.

14. Peter Keating anaendelea kumtishia, kumtetemesha na kumwogoposha huku Heyer akizidi kusisitiza asifanye hivyo.

15. Lucius Heyer anapata stroki anaanguka chini na kufariki na Peter Keating anafanikiwa kuandika wosia kwa niaba yake.

16. Guy Francon anamwambia Peter Keating kwamba wosia wa Lucius Heyer umesomwa asubuhi na kwamba amemwachia mali zake zote Peter Keating zikiwemo Estate kubwa lenye thamani ya milioni 500 na hisa zake za kampuni ya Francon & Heyer kwamba Lucius Heyer hakuwa na ndugu kabisa.

17. Nafsi inamhukumu Peter Keating kwamba amekuwa mbinafsi kwa yale aliyofanya lakini anajisemea mwenyewe kwamba kila mtu ni mbinafsi.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *