USANIFU MAJENGO NA UJENZI – 12

KITABU: FOUNTAINHEAD.

AUTHOR: AYN RAND.

1. Steven Mallory anampiga risasi Ellsworth Toohey lakini kwa bahati nzuri anamkosa na kukamatwa na polisi.

2. Ellsworth Toohey wanakutana na Peter Keating na kuongea mambo mengi kwa kirefu ofisini kwa Ellsworth Toohey, wanazingumzia pia tukio la jaribia kupigwa risasi Ellsworth Toohey.

3. Ellsworth Toohey anamwambia Peter Keating kwamba anahisi Steven Mallory ni mtu asiye na uwezo na pengine aliwahi kufanya ukosoaji uliomuumiza, lakini yeye binafsi hamjui wala hajawahi kumwona Steven Mallory hapo kabla.

4. Mwisho wanazingumzia mahusiano yake Peter Keating na Catherine. Ellsworth Toohey anasema anakubaliana kabisa na mahusiano yao na ndoa yao na Catherine japo Peter Keating anahisi kuna hisia asizozielewa kwa Ellsworth Toohey juu ya jambo hilo.

5. Peter Keating anapewa kazi ya kufanya design ya jengo na Miss Lois Cook. Miss Lois Cook anamwambia anataka afanye design ya jengo baya kuliko yote New York. 6. Dominique amerudi New York baada ya kutembelea mgodi kwa siku tatu zaidi.

7. Dominique anakutana na Ellsworth Toohey wanazungumza kwa kiasi. Dominique anaona mchoro wa mkato(section) ya jengo la nyumba ya Roger Enright na analipenda sana.

8. Dominique anasema huyo mtu aliyefanya design ya jengo la Roger Enright hatakiwi kuruhusu lijengwe.

9. Steven Mallory anagoma kabisa kutoa sababu mahakamani ya nini kilichomsukuma kujaribu kumpiga risasi Ellsworth Toohey. Hakika anampa adhabu ya kifungo cha miaka miwili gerezani.

10. Ellsworth Toohey anaanzisha chama cha wasanifu majengo pamoja na wanataaluma wengine wanaoendana nayo na wanafanya mkutano wa kwanza.

11. Dominique anahudhuria mkutano huo kwa ghafla bila mwaliko wala kujulikana kama atakuwepo. Huko anakutana na Ellsworth Toohey, Peter Keating Gordon L. Prescott na watu wengine. Baada ya mkutano kumalizika Peter Keating anamfuata Dominique ambaye alikuwa anamtazama sana wakati mkutano ulipokuwa unaendelea.

12. Dominique anamuuliza Ellsworth Toohey kwa nini hawajamkaribisha yule mtu aliyefanya jengo la Roger Enright. Dominique anaulizia jina la huyo Msanifu anajibiwa kwamba anaitwa Howard Roark. Dominique hajawahi kusikia hilo jina.

13. Peter Keating anaendelea kuzungumza na Dominique na kushangaa imekuwaje amefika pale. Dominique anawaambia kwamba hategemei kuwa mwanachama wa chama chao wala kuhudhuria mkutano ujao.

14. Peter Keating anaita taxi wanapanda na Dominique na kuzungumza. Peter anazungumzia kuhusu kutoweka kwa Dominique na kumwambia kwamba anampenda sana na hatakubali kumwachia atoweke tena.

15. Dominique anamwambia Peter hategemei kuwa karibu sana naye na asimpigie simu. Watakuwa wakikutana tu. Dominique anamwambia Peter kwamba yeye ni moja mifano ya vitu anavyovidharau na kuvichukia sana duniani. Peter anamwambia kamwe hatakata tamaa juu yake.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +2557171452790

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *