USANIFU MAJENGO NA UJENZI – 18 OFISI YA UJENZI

KITABU: FOUNTAINHEAD.

AUTHOR: AYN RAND.

1. Hopton Stoddard ameshinda kesi mahakamani.

2. Howard Roark anatakiwa kulipa gharama za kufanya mabadiliko ya jengo hilo la hekalu la Hopton Stoddard.

3. Howard Roark anasema kwamba hatakata rufaa kwa kesi hiyo.

4. Hopton Stoddard anatangaza kwamba jengo hilo linabadilishwa na kuwa nyumbani kwa watoto wenye matatizo maalum.

5. Catherine anazungumza na mjomba wake Ellsworth Toohey na kumwambia kwamba amefanya kazi za kujitolea lakini hajisikii tena kuwa na furaha kama alivyoahidiwa. Ellsworth Toohey anamwambia tatizo lake ni kwamba anajali sana furaha yake badala ya kujali kuhusu wengine.

6. Peter Keating anaenda nyumbani kwa Ellsworth Toohey kumwona Catherine. Peter anamwambia Catherine kwamba amefanya jambo la hovyo linaloonekana kuhusiana na Stoddard temple na anamwomba amsamehe bila hata kujua kosa lake. Catherine anamwambia amemsamehe.

7. Peter Keating anamwambia Catherine kwamba anahitaji kumuoa sasa. Anamwambia itabidi aache kazi na yeye aende kuchukua likizo ofisini waende nje ya mji wafunge ndoa. Peter Keating anamwambia Catherine Halsey ajiandae kesho kutwa yake anakuja amkute yuko tayari asubuhi waondoke.

8. Peter anaondoka kisha anakutana na Dominique wanaongea. Dominique anamwambia Peter yuko tayari sasa na amekubali kuolewa, lakini kwa masharti kwamba amuoe sasa hivi. Anamtaka waondoke siku hiyo hiyo kwenda nje ya New York huko Connecticut wakafunge ndoa.

9. Peter Keating anashangaa na kusita anabaki njia panda. Dominique anamshinikiza Peter kwamba ni aidha amuoe sasa hivi au amsahau kabisa, anasema kama hatamuoa sasa hivi basi hatampa tena hiyo nafasi, hivyo aamue ndio au hapana.

10. Peter Keating anakubaliana na Dominique kuhusu kufunga ndoa. Wanaondoka wawili Dominique anaendesha gari wanaelekea Connecticut nje ya New York.

11. Peter Keating na Dominique wanafunga ndoa kimya kimya nje ya New York.

12. Taarifa zinasambaa kila kona ya New York juu ya ndoa ya Peter Keating and Dominique Francon. Watu wanampigia sana simu Peterson Keating za pongezi juu ya hatua ya kumuoa binti mrembo na mwenye hadhi ya juu Dominique Francon.

13. Mama yake Peter Keating anafurahi sana, anakuwa na furaha kubwa kupitiliza kwa mtoto wake kumuoa Dominique Francon.

14. Peter Keating anamwacha Catherine kwenye mataa na wala hakumwambia kwamba amebadili mawazo na kuamua kumuoa Dominique Francon.

15. Dominique alifika ofisini kwa Howard Roark na kumwambia kwamba ameamua kuolewa na Peter Keating ikiwa ni sehemu ya kujiadhibu yeye mwenyewe.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *