USANIFU MAJENGO NA UJENZI – 19 MICHORO NA RAMANI KUREKEBISHWA

KITABU: FOUNTAINHEAD.

AUTHOR: AYN RAND.

1. Guy Francon anajivunia sana Peter Keating, anajaribu kuzungumzia kwamba astaafu na kumwachia kampuni Peter Keating moja kwa. Hata hivyo Peter Keating haonekani kulifurahia hilo.

2. Peter Keating na Dominique Francon wanatembelewa sana na wageni nyumbani kwao.

3. Ellsworth Toohey naye anawatembelea Peter Keating na Dominique nyumbani kwao. Peter Keating anaondoka na kuelekea ofisini. Ellsworth Toohey anamwambia Dominique mbona ameolewa na Peter Keating wakati hampendi. Ellsworth Toohey anamwambia Dominique kwamba anampenda Howard Roark na alianza kumpenda siku ile walipokutana kwenye sherehe ya Kiki Holcombe na kwamba Dominique alitamani kulala na Howard Roark siku hiyo hiyo. Dominique alibaki anashangaa jinsi Ellsworth Toohey aliweza kufahamu hilo kwa uhakika.

4. Hopton Stoddard anaongezea pesa nyingi kwenye ule mradi wa hekalu kwa ajili ya marekebisho juu ya ile hela iliyolipwa na Howard Roark.

5. Hekalu la Hopton Stoddard linajengwa kwa ajili ya kazi yake mpya ya kuwa kituo cha watoto wenye matatizo maalum. Wataalamu husika wa kujenga upya jengo hilo wanachaguliwa na Ellsworth Toohey.

6. Wasanifu majengo wanne waliochaguliwa na Ellsworth Toohey ni Peter Keating, Gordon L. Prescott, John Erik Snyte na kijana mdogo anayeitwa Gus Webb.

7. Umaarufu wa Ellsworth Toohey unaongezeka sana baada ya kesi ile dhidi ya Howard Roark. Hivyo na taasisi aliyoianzisha ya “the Council of America Buiders” inakuwa na kupata wanachama wengi sana.

8. Gail Wynand anaagiza Dominique afukuzwe kazi kwenye kampuni yake kutokana na maandiko yake yasiyoendana nao.

9. Jengo la Hopton Stoddard linakuwa ni jengo kubwa zaidi la ghorofa tano. Jengo hilo linajumuisha mabweni, madarasa, jiko, maeneo ya kufulia nguvu n.k.

10. Watoto wengi wameletwa kwenye kituo hicho cha Hopton Stoddard cha watoto wenye matatizo maalum kutoka maeneo mbalimbali.

11. Catherine Halsey anaingia kufanya kazi kwenye kituo hicho. Catherine anahamia moja kwa moja katika jengo hilo na kujivunia kufanya kazi hapo.

12. Bilionea Gail Wynand ameshika bastola na anafikiria kujiuwa lakini anasita. Anaona hilo sio jambo sahihi kufanya kwa wakati huu.

13. Ellsworth Toohey wanazungumza na Gail Wynand ofisini kwake, na Gail Wynand anafikiri anaweza kuwadhibiti wafanyakazi wake au watoa huduma wake kiurahisi.

Ahsanteni.

Karibu sana.

Architect Sebastian Moshi.

Whatsapp/Call +255717452790.

0 replies

Leave a Reply

Want to join the discussion?
Feel free to contribute!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *